Miriamu Na Aroni Wampinga Mose
1 Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi.
2 Waliuliza, “Je,Bwanaamesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” NayeBwanaakasikia hili.
3 (Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine ye yote katika uso wa dunia.)
4 GhafulaBwanaakawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njoni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda.
5 KishaBwanaakashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele,
6 Bwanaakasema, “Sikilizeni maneno yangu:
“Akiwapo nabii waBwanamiongoni mwenu,
nitajifunua kwake kwa maono,
nitanena naye katika ndoto.
7 Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;
yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.
8 Kwake nitanena naye uso kwa uso,
waziwazi wala si kwa mafumbo;
yeye ataona umbo laBwana.
Kwa nini basi ninyi hamkuogopa
kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”
9 Hasira yaBwanaikawaka dhidi yao, akawaacha.
10 Wakati hilo wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia akaona ana ukoma;
11 akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu.
12 Usimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”
13 Hivyo Mose akamliliaBwanaakisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”
14 Bwanaakamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.”
15 Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.
16 Baada ya hayo, watu waliondoka Haserothi, wakapiga kambi katika Jangwa la Parani.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/12-ca41a1439e1a5ac5eca1313dc61c6e01.mp3?version_id=1627—