Isaya 31

Ole Wa Wale Wanaotegemea Misri

1 Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada,

wale wategemeao farasi,

wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita

na katika nguvu nyingi za wapanda farasi,

lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

wala hawatafuti msaada kwaBwana.

2 Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa,

wala hayatangui maneno yake.

Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu,

dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya.

3 Lakini Wamisri ni wanadamu wala si Mungu,

farasi wao ni nyama wala si roho.

WakatiBwanaatakaponyosha Mkono wake,

yeye anayesaidia atajikwaa,

yeye anayesaidiwa ataanguka,

wote wawili wataangamia pamoja.

4 Hili ndiloBwanaanaloniambia:

“Kama vile simba angurumavyo,

simba mkubwa juu ya mawindo yake:

hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo

huitwa pamoja dhidi yake,

hatiwi hofu na kelele zao

wala kusumbuliwa na ghasia zao;

ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote atakavyoshuka

kufanya vita juu ya Mlima Sayuni

na juu ya vilele vyake.

5 Kama ndege warukao,

BwanaMwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu;

ataukinga na kuuokoa,

atapita juu yake na kuufanya salama.”

6 Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana.

7 Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.

8 “Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu;

upanga, ambao si wa kibinadamu,

utawaangamiza.

Watakimbia mbele ya upanga

na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.

9 Ngome zao zitaanguka kwa sababu ya hofu,

kwa kuona bendera ya vita,

majemadari wao watashikwa na hofu ya ghafula,”

asemaBwana,

ambaye moto wake uko Sayuni,

nayo tanuru yake iko Yerusalemu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/31-5cfb50d7e1913a2e11ccab7e3b674f51.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × four =