Yeremia 42

Yeremia Ashauri Walionusurika Wasihame Yuda

1 Ndipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea na Yezania mwana wa Hoshaya na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia

2 Yeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombeBwanaMungu wako kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa kama unavyoona sasa, ingawa wakati fulani tulikuwa wengi, sasa ni wachache tu waliosalia.

3 Omba iliBwanaMungu wako atuambie tuende wapi na tufanye nini.”

4 Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwombaBwanaMungu wenu kama mlivyoomba, nitawaambia kila kitu asemachoBwanawala sitawaficha cho chote.”

5 Kisha wakamwambia Yeremia, “Bwanana awe shahidi wa kweli na mwaminifu juu yetu kama hatutafanya sawasawa na kila kituBwanaMungu wako atakachokutuma utuambie.

6 Likiwa jema au likiwa baya, tutamtiiBwanaMungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtiiBwanaMungu wetu.”

7 Baada ya siku kumi, neno laBwanalikamjia Yeremia.

8 Kwa hiyo akawaita pamoja Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye na watu wote kuanzia mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana.

9 Akawaambia, “Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kuwasilisha maombi yenu, asema:

10 ‘Kama mkikaa katika nchi hii, nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawang’oa, kwani ninahuzunishwa na maafa niliyowapiga nayo.

11 Msimwogope mfalme wa Babeli, ambaye sasa mnamwogopa. Msimwogope, asemaBwana, kwa kuwa niko pamoja nanyi nami nitawaokoa na kuwaponya kutoka mikononi mwake.

12 Nitawaonea huruma ili naye awe na huruma juu yenu na kuwarudisha ninyi katika nchi yenu.’

13 “Hata hivyo, kama mkisema, ‘Hatutakaa katika nchi hii,’ hivyo mkaacha kumtiiBwanaMungu wenu,

14 nanyi kama mkisema, ‘Hapana, tutakwenda kuishi Misri, mahali ambapo hatutaona vita au kusikia sauti ya tarumbeta au kuwa na njaa ya chakula,’

15 basi sikieni neno laBwana, enyi mabaki ya Yuda. Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Ikiwa mmekusudia kwenda Misri na kufanya makazi huko,

16 basi ule upanga mnaouogopa utawapata huko na njaa mnayoihofia itawafuata huko Misri, nanyi mtafia huko.

17 Naam, wote waliokusudia kwenda kuishi Misri watakufa kwa upanga, njaa na tauni; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika au kuokoka maafa nitakayoyaleta juu yao.’

18 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama vile hasira yangu na ghadhabu yangu ilivyomwagwa juu ya wale walioishi Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu mtakapokwenda Misri. Mtakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha kulaumia na cha kushutumia, nanyi kamwe, hamtaona mahali hapa tena.’

19 “Enyi mabaki ya Yuda,Bwanaamewaambia, ‘Msiende Misri.’ Hakikisheni jambo hili: Ninawaonya leo

20 kwamba mmefanya kosa kubwa mioyoni mwenu mliponituma kwaBwanaMungu wenu na kusema, ‘MwombeBwanaMungu wetu kwa ajili yetu, nawe utuambie kila kitu atakachosema, nasi tutafanya.’

21 Nimewaambieni leo, lakini bado ninyi hamtaki kumtiiBwanaMungu wenu katika yote aliyonituma mimi niwaambie.

22 Basi sasa, hakikisheni jambo hili: Mtakufa kwa upanga, njaa na tauni mahali ambapo mnataka kwenda kuishi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/42-cbf1b9b5829e6b57663bebfd3101cb3a.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 − 14 =