Upendo Wa Mungu
(Zaburi Ya Daudi)
1 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana,
vyote vilivyomo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu.
2 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana,
wala usisahau wema wake wote,
3 akusamehe dhambi zako zote,
akuponya magonjwa yako yote,
4 aukomboa uhai wako na kaburi,
akuvika taji ya upendo na huruma,
5 atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema,
ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.
6 Bwanahutenda haki,
naye huwapa hukumu ya haki
wote wanaoonewa.
7 Alimjulisha Mose njia zake,
matendo yake kwa wana wa Israeli.
8 Bwanani mwenye huruma na rehema,
si mwepesi wa hasira,
amejaa upendo.
9 Yeye hatalaumu siku zote,
wala haweki hasira yake milele,
10 yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu
wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.
11 Kama vile mbingu zilivyo juu sana juu ya dunia,
ndivyo wema wake ulivyo mwingi
kwa wanaomcha;
12 kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo Mungu alivyoziweka
dhambi zetu mbali nasi.
13 Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyoBwanaanavyowahurumia
wale wanaomcha;
14 kwa kuwa anajua tulivyoumbwa,
anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.
15 Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani,
anachanua kama ua la shambani;
16 upepo huvuma juu yake nalo hutoweka,
mahali pake hapalikumbuki tena.
17 Lakini kutoka milele hata milele
upendo waBwanauko kwa wale wamchao,
nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:
18 kwa wale walishikao Agano lake
na kukumbuka kuyatii mausia yake.
19 Bwanaameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni,
ufalme wake unatawala juu ya vyote.
20 MhimidiniBwana, enyi malaika zake,
ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake,
ninyi mnaotii neno lake.
21 MhimidiniBwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni,
ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake.
22 MhimidiniBwana, kazi zake zote
kila mahali katika milki yake.
Ee nafsi yangu, umhimidiBwana.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/103-27ce97ceb3011e92f6a21ca1ee3d567b.mp3?version_id=1627—