Zaburi 109

Lalamiko La Mtu Aliyeko Kwenye Shida

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

1 Ee Mungu, ambaye ninakusifu,

usiwe kimya,

2 kwa maana watu waovu na wadanganyifu

wamefungua vinywa vyao dhidi yangu;

wasema dhidi yangu

kwa ndimi za udanganyifu.

3 Wamenizunguka kwa maneno ya chuki,

wananishambulia bila sababu.

4 Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki,

lakini mimi ninawaombea.

5 Wananilipiza baya kwa jema,

chuki badala ya urafiki wangu.

6 Agiza mtu mwovu ampinge,

# mshtakina asimame mkono wake wa kuume.

7 Anapohukumiwa na apatikane na hatia,

nayo maombi yake na yamhukumu.

8 Siku zake za kuishi na ziwe chache,

uongozi wake na apewe mtu mwingine.

9 Watoto wake na waachwe yatima,

mke wake na awe mjane.

10 Watoto wake na watangetange wakiomba-omba,

na wafukuzwe kwenye magofu

ya nyumba zao zilizobomoka.

11 Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo,

matunda ya kazi yake

na yatekwe nyara na wageni.

12 Asiwepo mtu ye yote wa kumtendea mema

wala wa kuwahurumia yatima wake.

13 Uzao wake na ukatiliwe mbali,

majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.

14 Maovu ya baba zake na yakumbukwe

mbele zaBwana,

dhambi ya mama yake

na isifutwe kamwe.

15 Dhambi zao na zibaki daima mbele zaBwana,

ili apate kukatilia mbali

kumbukumbu lao duniani.

16 Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema,

bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,

aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.

17 Alipenda kulaani,

nayo laana ikampata;

hakupenda kubariki,

kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.

18 Alivaa kulaani kama vazi lake,

nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji,

kwenye mifupa yake kama mafuta.

19 Na iwe kama joho alilozungushiwa,

kama mshipi aliofungiwa daima.

20 Haya na yawe malipo yaBwana

kwa washtaki wangu,

kwa wale wanaoninenea mabaya.

21 Lakini wewe, EeBwanaMwenyezi,

unitendee wema kwa ajili ya jina lako,

uniokoe kwa wema wako.

22 Maana mimi ni maskini na mhitaji,

moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.

23 Ninafifia kama kivuli cha jioni,

nimerushwa-rushwa kama nzige.

24 Magoti yangu yamelegea kwa kufunga,

mwili wangu umedhoofika na kukonda.

25 Nimekuwa kitu cha kudharauliwa

kwa washtaki wangu,

wanionapo, hutikisa vichwa vyao.

26 EeBwana, Mungu wangu nisaidie,

niokoe sawasawa na upendo wako.

27 Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako,

kwamba wewe, EeBwana,

umetenda hili.

28 Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki,

watakaposhambulia wataaibishwa,

lakini mtumishi wako atashangilia.

29 Washtaki wangu watavikwa fedheha,

na kufunikwa na aibu kama joho.

30 Kwa kinywa changu nitamtukuza sanaBwana

katika umati mkubwa nitamsifu.

31 Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji,

kuokoa maisha yake

kutoka kwa wale wanaomhukumu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/109-fd72b023db33f14ecb3b7e5a63785879.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × 4 =