Maajabu Ya Mungu Wakati Israeli Walipotoka Misri
1 Wakati Israeli walipotoka Misri,
nyumba ya Yakobo
kutoka kwa watu wa lugha ngeni,
2 Yuda akawa makao matakatifu ya Mungu,
Israeli akawa milki yake.
3 Bahari ilitazama ikakimbia,
Yordani ulirudi nyuma,
4 milima ilirukaruka kama kondoo waume,
vilima kama wana-kondoo.
5 Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,
Ee Yordani, nawe ukarudi nyuma,
6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo waume,
enyi vilima, kama wana-kondoo?
7 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana,
mbele za Mungu wa Yakobo,
8 yeye aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,
mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/114-a52b5ed5bf63e707f5cbb4eefbbfdc14.mp3?version_id=1627—