Kuomba Msaada
(Wimbo Wa Kwenda Juu)
1 Katika dhiki yangu namwitaBwana,
naye hunijibu.
2 EeBwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.
3 Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi,
Ewe ulimi mdanganyifu?
4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka
ya mti wa mretemu.
5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati
ya hema za Kedari!
6 Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale
wanaochukia amani.
7 Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema,
wao wanataka vita.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/120-df46a67e829af36a3dad513361f137eb.mp3?version_id=1627—