Shukrani Kwa Ukombozi Wa Israeli
(Wimbo Wa Kwenda Juu)
1 KamaBwanaasingalikuwa upande wetu;
Israeli na aseme sasa:
2 kamaBwanaasingalikuwa upande wetu,
wakati watu walipotushambulia,
3 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,
wangalitumeza tungali hai,
4 Mafuriko yangalitugharikisha,
maji mengi yangalitufunika,
5 maji yaendayo kasi
yangalituchukua.
6 Bwanaasifiwe,
yeye ambaye hakuruhusu
turaruliwe kwa meno yao.
7 Tumeponyoka kama ndege
kutoka katika mtego wa mwindaji;
mtego umevunjika,
nasi tukaokoka.
8 Msaada wetu ni katika jina laBwana,
Muumba wa mbingu na dunia.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/124-9ccb6bbd9ae29a84ffb8315500236917.mp3?version_id=1627—