Usalama Wa Watu Wa Mungu
(Wimbo Wa Kwenda Juu)
1 Wale wamtumainioBwanani kama mlima Sayuni,
ambao hauwezi kutikisika wadumu milele.
2 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,
ndivyoBwanaanavyowazunguka watu wake
sasa na hata milele.
3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi
waliopewa wenye haki,
ili kwamba wenye haki wasije
wakatumia mikono yao
kutenda ubaya.
4 EeBwana, watendee mema walio wema,
wale walio wanyofu wa moyo.
5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,
Bwanaatawafukuza
pamoja na watenda mabaya.
Amani iwe juu ya Israeli.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/125-370cee1374973ac54166d030d902839e.mp3?version_id=1627—