Kuomba Msaada
(Wimbo Wa Kwenda Juu)
1 Kutoka katika vilindi ninakulilia, EeBwana,
2 EeBwana, sikia sauti yangu.
Masikio yako na yawe masikivu
kwa kilio changu unihurumie.
3 Kama wewe, EeBwana,
ungeweka kumbukumbu ya dhambi,
EeBwana, ni nani
angeliweza kusimama?
4 Lakini kwako kuna msamaha,
kwa hiyo wewe unaogopwa.
5 NamngojeaBwana, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
6 Nafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
7 Ee Israeli, mtumainiBwana,
maana kwaBwanakuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli
kutoka katika dhambi zao zote.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/130-0fa0927afafceabcb36aa675010cc524.mp3?version_id=1627—