Maombi Ya Shukrani
(Zaburi Ya Daudi)
1 Nitakusifu wewe, EeBwana,
kwa moyo wangu wote,
mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako.
2 Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu,
nami nitalisifu jina lako
kwa ajili ya upendo wako
na uaminifu,
kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako
juu ya vitu vyote.
3 Nilipoita, ulinijibu;
ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.
4 Wafalme wote wa dunia,
na wakusifu wewe EeBwana,
wakati wanaposikia
maneno ya kinywa chako.
5 Wao na waimbe kuhusu njia zaBwana,
kwa maana utukufu waBwanani mkuu.
6 IngawaBwanayuko juu,
humwangalia mnyonge,
bali mwenye kiburi
yeye anamjua kutokea mbali.
7 Nijapopita katikati ya shida,
wewe unayahifadhi maisha yangu,
unanyosha mkono wako
dhidi ya hasira ya adui zangu,
kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.
8 Bwanaatatimiza kusudi lake kwangu,
EeBwana, upendo wako wadumu milele:
usiziache kazi za mikono yako.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/138-d40040723c8c708f47c1cf84d80d04cd.mp3?version_id=1627—