Zaburi 32

Furaha Ya Msamaha

(Utenzi: Zaburi Ya Daudi. Funzo)

1 Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,

ambaye dhambi zake zimefunikwa.

2 Heri mtu yule ambayeBwana

hamhesabii dhambi,

na ambaye rohoni mwake

hamna udanganyifu.

3 Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa

kwa kulia kwa maumivu makali

mchana kutwa.

4 Usiku na mchana mkono wako ulinilemea,

nguvu zangu zilinyonywa

kama vile katika joto la kiangazi.

5 Kisha nilikujulisha dhambi yangu

wala sikuficha uovu wangu.

Nikasema, “Nitaungama

makosa yangu kwaBwana,”

ndipo uliponisamehe

hatia ya dhambi yangu.

6 Kwa hiyo kila mtu mtauwa na akuombe

maadamu unapatikana,

hakika maji makuu yatakapofurika

hayatamfikia yeye.

7 Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,

utaniepusha na taabu

na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

8 Nitakufundisha na kukuonyesha

njia utakayoiendea;

nitakushauri na kukuangalia.

9 Usiwe kama farasi au nyumbu

wasio na akili,

ambao ni lazima waongozwe

kwa lijamu na hatamu

la sivyo hawatakukaribia.

10 Mtu mwovu ana taabu nyingi,

bali upendo usio na kikomo waBwana

unamzunguka mtu anayemtumaini.

11 Shangilieni katikaBwanana mfurahi,

enyi wenye haki!

Imbeni, ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/32-6087b1c971c45e990043259d2e9cb7ac.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seven + 1 =