Zaburi 33

Ukuu Na Wema Wa Mungu

1 MwimbieniBwanakwa furaha, enyi wenye haki;

kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.

2 MsifuniBwanakwa kinubi,

mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.

3 Mwimbieni wimbo mpya;

pigeni kwa ustadi,

pigeni kelele za furaha.

4 Maana neno laBwanani haki na kweli,

ni mwaminifu kwa yote atendayo.

5 Hupenda uadilifu na haki;

dunia imejaa upendo wake usiokoma.

6 Kwa neno laBwanambingu ziliumbwa,

jeshi lao la angani

kwa pumzi ya kinywa chake.

7 Ameyakusanya maji ya bahari

kama kwenye mtungi;

vilindi vya bahari

ameviweka katika ghala.

8 Dunia yote na imwogopeBwana,

watu wote wa dunia wamche.

9 Kwa maana Mungu alisema, na ikawa,

aliamuru na ikasimama imara.

10 Bwanahuzuia mipango ya mataifa,

hupinga makusudi ya mataifa.

11 Lakini mipango yaBwana

inasimama imara milele,

makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.

12 Heri taifa ambaloBwanani Mungu wao,

watu ambao aliwachagua

kuwa urithi wake.

13 Kutoka mbinguniBwanahutazama chini

na kuwaona wanadamu wote;

14 kutoka maskani mwake huwaangalia

wote wakaao duniani,

15 yeye ambaye huumba mioyo yao wote,

ambaye huangalia

kila kitu wanachokitenda.

16 Hakuna mfalme aokokaye

kwa ukubwa wa jeshi lake;

hakuna shujaa aokokaye

kwa wingi wa nguvu zake.

17 Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu,

licha ya nguvu zake nyingi hawezi kuokoa.

18 Lakini macho yaBwanayako kwa wale wamchao,

kwa wale ambao tumaini lao

ni katika upendo wake usio na kikomo,

19 ili awaokoe na mauti,

na kuwahifadhi wakati wa njaa.

20 Sisi tunamngojeaBwanakwa matumaini,

yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

21 Katika yeye mioyo yetu hushangilia,

kwa maana tunalitumainia

jina lake takatifu.

22 Upendo wako usio na mwisho

ukae juu yetu, EeBwana,

kama vile tunavyoweka

tumaini letu kwako.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/33-1fce9b791359e502eb1f99b6a9c33f07.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 + one =