Sifa Na Wema Wa Mungu
(Zaburi Ya Daudi, Alipojifanya Mwendawazimu Mbele Ya Abimeleki, Ambaye Alimfukuza, Naye Akaondoka)
1 NitamtukuzaBwananyakati zote,
sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
2 Nafsi yangu itajisifu katikaBwana
walioonewa wasikie na wafurahi.
3 MtukuzeniBwanapamoja nami,
naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
4 NilimtafutaBwananaye akanijibu,
akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
5 Wale wamtazamao hutiwa nuru,
nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
6 Maskini huyu alimwitaBwanaakamsikia,
akamwokoa katika taabu zake zote.
7 Malaika waBwanahufanya kituo
akiwazunguka wale wamchao,
naye huwaokoa.
8 Onjeni mwone kwambaBwanani mwema,
heri mtu yule anayemkimbilia.
9 McheniBwanaenyi watakatifu wake,
kwa maana wale wamchao
hawapungukiwi na kitu cho chote.
10 Wana simba wenye nguvu
hutindikiwa na kuona njaa,
bali wale wamtafutaoBwana
hawatakosa kitu cho chote kilicho chema.
11 Njoni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumchaBwana.
12 Ye yote kati yenu anayependa maisha
na kutamani kuziona siku nyingi njema,
13 auzuie ulimi wake na mabaya
na midomo yake kutokana
na kusema uongo.
14 Aache uovu na atende mema,
aitafute amani na kuifuatia.
15 Macho yaBwanayako kwa wenye haki
na masikio yake yako makini
kusikia kilio chao;
16 uso waBwanauko kinyume na watenda mabaya,
kufuta kumbukumbu lao duniani.
17 Wenye haki hulia, nayeBwanahuwasikia,
huwaokoa katika taabu zao zote.
18 Bwanayu karibu nao waliovunjika moyo
na huwaokoa waliopondeka roho.
19 Mwenye haki ana mateso mengi,
lakiniBwanahumwokoa nayo yote,
20 huhifadhi mifupa yake yote,
hata mmoja hautavunjika.
21 Ubaya utamwua mtu mwovu,
adui za mwenye haki watahukumiwa.
22 Bwanahuwakomboa watumishi wake,
wale wanaomkimbilia yeye
hawatahukumiwa hata mmoja wao.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/34-ccb420443dc43577cc3db3894086b01d.mp3?version_id=1627—