Zaburi 41

Maombi Ya Mtu Mgonjwa

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

1 Heri mtu yule anayemjali mnyonge,

Bwanaatamwokoa wakati wa shida.

2 Bwanaatamlinda na kuyahifadhi maisha yake,

atambariki katika nchi

na hatamwacha katika tamaa ya adui zake.

3 Bwanaatamtegemeza awapo mgonjwa kitandani,

atamwinua kutoka kitandani mwake.

4 Nilisema, “EeBwananihurumie,

niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”

5 Adui zangu wanasema kwa hila,

“Lini atakufa na jina lake litokomee kabisa.”

6 Kila anapokuja mtu kunitazama,

huzungumza uongo,

huku moyo wake hukusanya masingizio;

kisha huondoka na kuyasambaza huko na huko.

7 Adui zangu wote hunong’onezana dhidi yangu,

hao huniwazia mabaya sana, wakisema,

8 “Ugonjwa mbaya sana umempata,

kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”

9 Hata rafiki yangu wa karibu, niliyemwamini,

yule aliyekula chakula changu

ameniinulia kisigino chake.

10 Lakini wewe, EeBwana, unihurumie,

ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.

11 Najua kwamba wapendezwa nami,

kwa kuwa adui yangu hanishindi.

12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza

na kuniweka kwenye uwepo wako milele.

13 MsifuniBwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Amen na Amen.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/41-e49091db6bebff4e9f22e709b3efe730.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × 3 =