Zaburi 42

Maombi Ya Mtu Aliye Uhamishoni

(Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Wana Wa Kora)

1 Kama vile paa aoneavyo shauku vijito vya maji,

ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu.

2 Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai.

Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?

3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu

mchana na usiku,

huku watu wakiniambia mchana kutwa,

“Yuko wapi Mungu wako?”

4 Vitu hivi ninavikumbuka

ninapoimimina nafsi yangu:

Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu,

nikiongoza maandamano

kuelekea kwenye nyumba ya Mungu,

kwa kelele za shangwe na za shukrani

katikati ya umati wa watu

wanaoadhimisha sikukuu.

5 Ee nafsi yangu kwa nini unasononeka?

Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?

Weka tumaini lako kwa Mungu,

kwa sababu bado nitamsifu,

aliye afya ya uso wangu

Mwokozi wangu na

6 Mungu wangu.

Nafsi yangu inasononeka ndani yangu;

kwa hiyo nitakukumbuka

kutoka nchi ya Yordani,

katika vilele vya Hermoni,

kutoka Mlima Mizari.

7 Kilindi huita kilindi,

katika ngurumo za maporomoko ya maji yako;

mawimbi yako yote pamoja na viwimbi

vimepita juu yangu.

8 MchanaBwanahuelekeza upendo wake,

usiku wimbo wake uko nami:

maombi kwa Mungu wa uzima wangu.

9 Ninamwambia Mungu Mwamba wangu,

“Kwa nini umenisahau?

Kwa nini niendelee kuomboleza,

nikiwa nimeonewa na adui?”

10 Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali

adui zangu wanaponidhihaki,

wakiniambia mchana kutwa,

“Yuko wapi Mungu wako?”

11 Ee nafsi yangu kwa nini unasononeka?

Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?

Weka tumaini lako kwa Mungu,

kwa sababu bado nitamsifu,

aliye afya ya uso wangu,

Mwokozi wangu na Mungu wangu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/42-b22cac1a8003a7912ce1f01e13fe83ca.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twenty − twelve =