Mtawala Mwenye Enzi Yote
(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora)
1 Pigeni makofi, enyi mataifa yote,
mpigieni Mungu kelele za shangwe!
2 Jinsi gani alivyo wa kutisha,BwanaAliye Juu Sana,
Mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3 Ametiisha mataifa chini yetu
na mataifa chini ya miguu yetu.
4 Alituchagulia urithi wetu kwa ajili yetu
fahari ya Yakobo, aliyempenda.
5 Mungu amepaa katikati ya kelele za shangwe,
Bwanakatikati ya sauti za tarumbeta.
6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,
mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
7 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,
mwimbieni zaburi za sifa.
8 Mungu anatawala juu ya mataifa,
Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
9 Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu,
kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu;
yeye ametukuka sana.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/47-e21b9683f9512765cfa2895d3ed9ceab.mp3?version_id=1627—