Utukufu Wa Mungu Na Heshima Ya Mwanadamu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Daudi)
1 EeBwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Umeuweka utukufu wako
juu ya mbingu.
2 Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao
umeweka sifa,
kwa sababu ya watesi wako,
kuwanyamazisha adui na mlipiza kisasi.
3 Nikiziangalia mbingu zako,
kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota,
ulizoziratibisha,
4 mwanadamu ni kitu gani hata umkumbuke,
binadamu hata umwangalie?
5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu,
umemvika taji ya utukufu na heshima.
6 Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;
umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, mbuzi na ng’ombe wote pia,
naam, na wanyama wa kondeni,
8 ndege wa angani na samaki wa baharini,
naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari.
9 EeBwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/8-9b9688e20a06c6dd7f5a4839406532c4.mp3?version_id=1627—