Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki
(Zaburi Ya Asafu)
1 Mungu anaongoza kusanyiko kuu,
anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki
na kuonyesha upendeleo kwa waovu?
3 Teteeni wanyonge na yatima,
tunzeni haki za maskini na walioonewa.
4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji,
wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
5 “Hawajui lo lote, hawaelewi lo lote.
Wanatembea gizani,
misingi yote ya dunia imetikisika.
6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;
ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’
7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;
mtaanguka kama mtawala mwingine ye yote.”
8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,
kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/82-60692687af86ed7e0cf29b48afb24c48.mp3?version_id=1627—