Kuionea Shauku Nyumba Ya Mungu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Wana Wa Kora)
1 EeBwanaMwenye Nguvu Zote,
makao yako yapendeza kama nini!
2 Nafsi yangu inatamani sana,
naam, hata kuona shauku,
kwa ajili ya nyua zaBwana;
moyo wangu na mwili wangu
vinamlilia Mungu Aliye Hai.
3 Hata shomoro amejipatia makao,
mbayuwayu amejipatia kiota
mahali awezapo kuweka makinda yake:
mahali karibu na madhabahu yako,
EeBwanaMwenye Nguvu Zote,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
4 Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,
wanaokusifu wewe daima.
5 Heri ni wale ambao nguvu zao ziko kwako,
na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
6 Wanapopita katika Bonde la Baka,
hulifanya mahali pa chemchemi,
# pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.
7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu,
hadi kila mmoja afikapo
mbele za Mungu huko Sayuni.
8 EeBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote,
sikia maombi yangu;
nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.
9 Ee Mungu, uitazame ngao yetu,
mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.
10 Siku moja katika nyua zako ni bora
kuliko siku elfu mahali pengine;
afadhali ningekuwa bawabu
katika nyumba ya Mungu wangu
kuliko kukaa katika mahema ya waovu.
11 Kwa kuwaBwanani jua na ngao,
Bwanahutoa wema na heshima;
hakuna kitu chema anachowanyima
wale ambao hawana hatia.
12 EeBwanaMwenye Nguvu Zote,
heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/84-de9fa6d217312710ae91c4f248286a9d.mp3?version_id=1627—