Zaburi 92

Wimbo Wa Kumsifu Mungu

(Zaburi: Wimbo Wa Sabato)

1 Ni vyema kumshukuruBwana

na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

2 kuutangaza upendo wako asubuhi,

uaminifu wako wakati wa usiku,

3 kwa zeze yenye nyuzi kumi

na kwa sauti ya kinubi.

4 EeBwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha,

nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.

5 EeBwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako,

tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!

6 Mjinga hafahamu,

mpumbavu haelewi,

7 ingawa waovu huchipua kama majani

na wote watendao mabaya wanastawi,

wataangamizwa milele.

8 Bali wewe, EeBwana,

utatukuzwa milele.

9 EeBwana, hakika adui zako,

hakika adui zako wataangamia,

wote watendao mabaya watatawanyika.

10 Umeitukuza pembeyangu kama ile ya nyati dume,

mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.

11 Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa,

masikio yangu yamesikia

maangamizi ya adui zangu waovu.

12 Wenye haki watastawi kama mtende,

watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,

13 waliopandwa katika nyumba yaBwana,

watastawi katika nyua za Mungu wetu.

14 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,

watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

15 wakitangaza, “Bwanani mkamilifu;

yeye ni Mwamba wangu,

na ndani yake hamna uovu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/92-abcb2c0bcc4264747d396a7aa8baa9d6.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − one =