Mungu Mfalme
1 Bwanaanatawala, amejivika utukufu;
Bwanaamejivika utukufu
tena amejivika nguvu.
Dunia imewekwa imara,
haitaondoshwa.
2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;
wewe umekuwako tangu milele.
3 Bahari zimeinua, EeBwana,
bahari zimeinua sauti zake;
bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.
4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Bwanaaishiye juu sana ni mkuu.
5 EeBwana, sheria zako ni imara;
utakatifu umepamba nyumba yako
pasipo mwisho.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/93-cf07080b63ce6141768c12b426ba7404.mp3?version_id=1627—