Wimbo Wa Kumsifu Mungu
1 Njoni, tumwimbieBwanakwa furaha;
tumfanyie kelele za shangwe
Mwamba wa wokovu wetu.
2 Tuje mbele zake kwa shukrani,
tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
3 Kwa kuwaBwanani Mungu mkuu,
mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4 Mkononi mwake mna vilindi vya dunia
na vilele vya milima ni mali yake.
5 Bahari ni yake, kwani ndiye aliyeifanya,
na mikono yake iliumba nchi kavu.
6 Njoni, tusujudu tumwabudu,
tupige magoti mbele zaBwanaMuumba wetu,
7 kwa maana yeye ndiye Mungu wetu
na sisi ni watu wa malisho yake,
kondoo chini ya utunzaji wake.
Kama mkiisikia sauti yake, leo,
8 msiifanye migumu mioyo yenu
# kama mlivyofanya kule Meriba,
kama mlivyofanya siku ile
# kule Masajangwani,
9 ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,
ingawa walikuwa wameyaona niliyoyafanya.
10 Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,
nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,
nao hawajazifahamu njia zangu.”
11 Kwa hiyo nikaapa katika hasira yangu,
“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/95-8b88b1c01eacb1139a02594f1d7bf3b8.mp3?version_id=1627—