Mungu Mtawala Wa Dunia
1 MwimbieniBwanawimbo mpya,
kwa maana ametenda mambo ya ajabu;
kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu
umemfanyia wokovu.
2 Bwanaameufanya wokovu wake ujulikane
na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.
3 Ameukumbuka upendo wake
na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;
miisho yote ya dunia imeuona
wokovu wa Mungu wetu.
4 Mpigieni kelele za shangwe, dunia yote,
ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
5 mwimbieniBwanakwa kinubi,
kwa kinubi na sauti za kuimba,
6 kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu
za pembe za kondoo dume:
shangilieni kwa furaha mbele zaBwana,
aliye Mfalme.
7 Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake,
dunia na wote wakaao ndani yake.
8 Mito na ipige makofi,
milima na iimbe pamoja kwa furaha,
9 vyote na viimbe mbele zaBwana,
kwa maana yuaja kuhukumu dunia.
Atahukumu dunia kwa haki
na mataifa kwa haki.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/98-7163a39f7828c4519ba46a2a4ee3a38a.mp3?version_id=1627—