Mungu Mfalme Mkuu
1 Bwanaanatawala,
mataifa na yatetemeke;
anaketi kwenye kiti cha enzi katikati ya makerubi,
dunia na itikisike.
2 Bwanani mkuu katika Sayuni;
ametukuzwa juu ya mataifa yote.
3 Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:
yeye ni mtakatifu!
4 Mfalme mwenye nguvu hupenda haki,
wewe umethibitisha adili;
katika Yakobo umefanya
yaliyo haki na sawa.
5 MtukuzeniBwanaMungu wetu,
na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;
yeye ni mtakatifu.
6 Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,
Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;
walimwita naye aliwajibu.
7 Alizungumza nao kutoka katika nguzo ya wingu;
walizishika sheria zake na amri alizowapa.
8 EeBwana, wetu,
ndiwe uliyewajibu,
kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,
ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.
9 MtukuzeniBwanaMungu wetu
na mwabudu kwenye mlima wake mtakatifu,
kwa maanaBwanaMungu wetu ni mtakatifu.
—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/99-11d9d4ae955a940aed5492da831339ad.mp3?version_id=1627—