Kumbukumbu La Torati 19

Miji Ya Makimbilio 1 WakatiBwanaMungu wenu atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakapokuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao, 2 ndipo mtenge miji mitatu iliyopo katikati ya nchi kwa ajili yenu, katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kuimiliki. 3 Jengeni barabara katika miji hiyo na kuigawa mara tatu, nchi anayowapaBwanaMungu […]

Kumbukumbu La Torati 20

Kwenda Vitani 1 Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababuBwanaMungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi. 2 Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi. 3 Atasema: “Sikia, Ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife […]

Kumbukumbu La Torati 21

Upatanisho Kuhusu Mauaji 1 Kama mtu akikutwa ameuawa, naye amelala kwenye shamba katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kuimiliki, wala haijulikani ni nani aliyemwua, 2 wazee wenu na waamuzi watatoka na kupima umbali kutoka maiti alipolala mpaka kwenye miji ya jirani. 3 Kisha wazee wa ule mji uliokaribu zaidi na yule maiti watamchukua mtamba ambaye hajapata […]

Kumbukumbu La Torati 26

Malimbuko Na Zaka 1 Mtakapokuwa mmeingia nchi ile ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi na mtakapokuwa mmeimiliki na kukaa ndani yake, 2 chukueni baadhi ya mavuno ya kwanza ya yale yote mtakayozalisha kutoka udongo wa nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa na mweke kwenye kapu. Kisha uende mahali ambapoBwanaMungu wako atapachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina lake […]

Kumbukumbu La Torati 27

Madhabahu Katika Mlima Ebali 1 Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo. 2 Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi awapayoBwanaMungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu. 3 Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayoBwanaMungu wenu, nchi itiririkayo […]