Kufanya Upya Agano 1 Haya ndiyo maneno ya AganoBwanaaliyomwagiza Mose kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya Agano alilofanya nao huko Horebu. 2 Mose akawaita Waisraeli wote akawaambia: Macho yenu yameona yale yoteBwanaaliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote. 3 Kwa macho yenu wenyewe mliona yale […]
Monthly Archives: July 2017
Kumbukumbu La Torati 30
Mafanikio Baada Ya Kumgeukia Bwana 1 Wakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popoteBwanaMungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa, 2 hapo wewe na watoto wako mtakapomrudiaBwanaMungu wako, na kumtii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kulingana na kila kitu ninachokuamuru leo, 3 ndipoBwanaMungu wako atakapokurudisha […]
Kumbukumbu La Torati 31
Yoshua Kutawala Baada Ya Mose 1 Kisha Mose akaenda akasema maneno haya kwa Waisraeli wote: 2 “Sasa nina miaka mia moja na ishirini nami siwezi tena kuwaongoza.Bwanaameniambia, ‘Hutavuka Yordani.’ 3 BwanaMungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kamaBwanaalivyosema. 4 NayeBwanaatawafanyia watu […]
Kumbukumbu La Torati 32
1 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema; sikia, ee nchi, maneno ya kinywa changu. 2 Mafundisho yangu na yanyeshe kama mvua, na maneno yangu na yashuke kama umande, kama manyunyu juu ya majani mabichi, kama mvua tele juu ya mimea myororo. 3 Nitalitangaza jina laBwana. Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu! 4 Yeye ni Mwamba, kazi […]
Kumbukumbu La Torati 33
Mose Anayabariki Makabila 1 Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. 2 Alisema: “Bwanaalikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka matelemko ya mlima wake. 3 Hakika ni wewe ambaye huwapenda […]
Kumbukumbu La Torati 34
Kifo Cha Mose 1 Kisha Mose akaupanda mlima Nebo kutoka tambarare za Moabu mpaka kilele cha Pisga, ng’ambo ya Yeriko. HukoBwanaakamwonyesha nchi yote: kutoka Gileadi mpaka Dani, 2 Naftali yote, nchi ya Efraimu na Manase, nchi yote ya Yuda mpaka bahari ya magharibi, 3 Negebu na nchi yote kuanzia Bonde la Yeriko, Mji wa Mitende, […]
Hesabu 1
Watu Wahesabiwa Kwa Mara Ya Kwanza 1 Bwanaalisema na Mose katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia, 2 “Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume […]
Hesabu 2
Mpangilio Wa Kambi Za Makabila 1 Bwanaaliwaambia Mose na Aroni: 2 “Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.” 3 Kwa upande wa mashariki kuelekea maawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya […]
Hesabu 3
Walawi 1 Hii ni hesabu ya jamaa ya Aroni na Mose kwa wakati uleBwanaalipozungumza na Mose, katika Mlima Sinai. 2 Majina ya wana wa Aroni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari. 3 Hayo yalikuwa majina ya wana wa Aroni, makuhani wapakwa mafuta, ambao walikuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani. 4 Hata hivyo […]
Hesabu 4
Wakohathi 1 Bwanaakawaambia Mose na Aroni, 2 “Wahesabu Wakohathi walio sehemu ya Walawi kwa koo zao na jamaa zao. 3 Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini wanaokuja kutumika katika kazi ya Hema la Kukutania. 4 “Hii ndiyo kazi ya Wakohathi katika Hema la Kukutania: Watatunza vitu vilivyo vitakatifu sana. 5 Wakati […]