Hesabu 5

Utakaso Wa Kambi 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu ye yote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao, au anayetokwa na majimaji ya aina yo yote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti. 3 Hii itakuwa ni kwa wote, yaani, wanaume na wanawake; watoeni nje ya […]

Hesabu 6

Mnadhiri 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili yaBwanakama Mnadhiri, 3 ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine cho chote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji […]

Hesabu 7

Sadaka Wakati Wa Kuweka Wakfu Maskani Ya Bwana 1 Mose alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuweka wakfu pamoja na vyombo vyake vyote. 2 Ndipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. 3 […]

Hesabu 8

Kuwekwa Kwa Taa 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Sema na Aroni umwambie, ‘Wakati utakapoziweka zile taa saba, zinatakiwa kuangaza eneo lililo mbele ya kinara cha taa.’ ” 3 Aroni akafanya hivyo; akaziweka zile taa ili zielekee mbele kwenye kinara cha taa, kama vileBwanaalivyomwamuru Mose. 4 Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia […]

Hesabu 9

Pasaka Huko Sinai 1 Bwanaakasema na Mose katika Jangwa la Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka Misri. Akasema, 2 “Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamuriwa. 3 Adhimisheni wakati ulioamuriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote […]

Hesabu 10

Tarumbeta Za Fedha 1 Bwanaakamwambia Mose: 2 “Tengeneza tarumbeta mbili za fedha ya kufua, uzitumie kwa kuita jumuiya pamoja na wakati wa kuvunja makambi ili kuondoka. 3 Tarumbeta zote mbili zikipigwa, jumuiya yote itakusanyika mbele yako katika ingilio la Hema la Kukutania. 4 Kama tarumbeta moja tu ikipigwa, viongozi, yaani wakuu wa koo za Israeli, […]

Hesabu 11

Moto Kutoka Kwa Bwana 1 Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwaBwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwaBwanaukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi. 2 Watu walipomlilia Mose, akamwombaBwana, nao moto ukazimika. 3 Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera, kwa sababu moto kutoka kwaBwanauliwaka miongoni mwao. Kware […]

Hesabu 12

Miriamu Na Aroni Wampinga Mose 1 Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 2 Waliuliza, “Je,Bwanaamesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” NayeBwanaakasikia hili. 3 (Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine ye yote katika uso wa […]

Hesabu 13

Kupeleleza Kanaani 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka katika kila kabila la baba zao tuma mmoja wa viongozi wao.” 3 Hivyo kwa agizo laBwanaMose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. 4 Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana […]

Hesabu 14

Watu Wanaasi 1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 2 Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! 3 Kwa niniBwanaanatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na […]