Hesabu 25

Moabu Yashawishi Israeli 1 Wakati Israeli alipokuwa akikaa Shitimu, wanaume wa Israeli walianza kuzini na wanawake wa Kimoabu, 2 ambao waliwaalika kushiriki katika kutoa kafara kwa miungu yao. Watu wakala na kusujudu mbele ya miungu hii. 3 Kwa hiyo Israeli akaungana katika kumwabudu Baali wa Peori. Hasira yaBwanaikawaka dhidi yao. 4 Bwanaakamwambia Mose, “Uwachukue viongozi […]

Hesabu 26

Kuhesabiwa Watu Mara Ya Pili 1 Baada ya hiyo tauni,Bwanaakamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, 2 “Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.” 3 Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya […]

Hesabu 27

Binti Wa Selofehadi 1 Binti za Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, walikuwa wa koo za Manase mwana wa Yosefu. Majina ya hao binti yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walikaribia 2 ingilio la Hema la Kukutania na kusimama mbele ya Mose, kuhani Eleazari, viongozi na kusanyiko […]

Hesabu 28

Sadaka Za Kila Siku 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’ 3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtoleaBwana: wana kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama […]

Hesabu 29

Sikukuu Ya Tarumbeta 1 “ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. 2 Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayoBwanaya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. […]

Hesabu 30

Nadhiri 1 Mose akawaambia viongozi wa makabila ya Israeli: “Hili ndiloBwanaanaloagiza: 2 Wakati mwanaume awekapo nadhiri kwaBwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema. 3 “Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwaBwana, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi, 4 na baba yake akasikia […]

Hesabu 31

Kulipiza Kisasi Juu Ya Wamidiani 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.” 3 Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi chaBwana. 4 Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.” 5 Kwa hiyo waliandaliwa […]

Hesabu 32

Makabila Ng’ambo Ya Yordani 1 Kabila la Wareubeni na Wagadi, ambao walikuwa na makundi makubwa ya ng’ombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo. 2 Hivyo walimjia Mose, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia, 3 “Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo […]

Hesabu 33

Vituo Katika Safari Ya Waisraeli 1 Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli wakati walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni. 2 Kwa agizo laBwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao: 3 Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya […]

Hesabu 34

Mipaka Ya Kanaani 1 Bwanaakamwambia Mose, 2 “Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo: 3 “ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, 4 […]