Msiwahukumu Wengine 1 Mkaribisheni yeye ambaye imani yake ni dhaifu, lakini si kwa kugombana na kubishana juu ya mawazo yake. 2 Mtu mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu, lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula mboga tu. 3 Yeye alaye kila kitu asimdharau yeye asiyekula. Wala yeye asiyekula kila kitu asimhukumu yule alaye […]
Monthly Archives: July 2017
Warumi 15
Usijipendeze Mwenyewe, Bali Wapendeze Wengine 1 Sisi tulio na nguvu, hatuna budi kuchukuliana na kushindwa kwa wale walio dhaifu wala si kujipendeza nafsi zetu wenyewe. 2 Kila mmoja wetu inampasa kumpendeza jirani yake kwa mambo mema, ili kumjenga katika imani. 3 Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe, bali kama ilivyoandikwa: “Matukano yao wale wanaokutukana wewe […]
Warumi 16
Salamu Kwa Watu Binafsi 1 Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea. 2 Naomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wo wote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao. 3 Wasalimuni Prisilana Akila, watumishi wenzangu katika Kristo Yesu. 4 Wao walihatarisha […]
Matendo 1
Ahadi Ya Roho Mtakatifu 1 Katika kitabu changu cha kwanza nilikuandikia mpendwa Theofilo, kuhusu mambo yote Yesu aliyofanya na kufundisha tangu mwanzo, 2 hadi siku ile alipochukuliwa kwenda mbinguni, baada ya kuwapa maelekezo kwa njia Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua. 3 Baada ya mateso yake, alijionyesha kwao na kuwathibitishia kwa njia nyingi kwamba yeye yu […]
Matendo 2
Kushuka Kwa Roho Mtakatifu 1 Ilipowadia siku ya Pentekoste, walikuwa wote mahali pamoja. 2 Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3 Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho […]
Matendo 3
Petro Amponya Mlemavu Kwa Jina La Yesu 1 Siku moja Petro na Yohana walikuwa wanapanda kwenda Hekaluni kusali yapata saa tisa alasiri. 2 Basi palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa. Alichukuliwa na kuwekwa kwenye lango la Hekalu liitwalo Zuri, kila siku ili aombe msaada kwa watu wanaoingia Hekaluni. 3 Huyu mtu akiwaona Petro […]
Matendo 4
Petro Na Yohana Mbele Ya Baraza 1 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wakisema na watu, makuhani, mkuu wa walinzi wa Hekalu na Masudakayo wakawajia wakiwa 2 wamekasirika sana kwa sababu hao mitume walikuwa wanawafundisha watu na kuhubiri kwamba katika Yesu kuna ufufuo wa wafu. 3 Wakawakamata Petro na Yohana na kuwatia gerezani mpaka kesho yake […]
Matendo 5
Anania Na Safira 1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. 2 Mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume. 3 Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na […]
Matendo 6
Saba Wachaguliwa Kuhudumia 1 Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, palitokea manung’uniko kati ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawanyo wa chakula wa kila siku. 2 Wale mitume kumi na wawili wakakusanya wanafunzi wote pamoja wakasema, “Haitakuwa vyema sisi kuacha huduma ya […]
Matendo 7
Hotuba ya Stefano 1 Ndipo Kuhani Mkuu akamwuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?” 2 Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa bado yuko Mesopotamia, kabla hajaishi Harani, 3 akamwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na kutoka kwa jamii yako uende katika nchi nitakayokuonyesha.’ 4 “Hivyo […]