Paulo Huko Korintho 1 Baada ya haya, Paulo akaondoka Athene akaenda Korintho. 2 Huko akakutana na Myahudi mmoja jina lake Akila, mwenyeji wa Ponto, ambaye alikuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona, 3 naye kwa kuwa alikuwa mtengeneza mahema kama wao, […]
Monthly Archives: July 2017
Matendo 19
Paulo Huko Efeso 1 Wakati Apolo akiwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, 2 akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” 3 Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yohana.” 4 Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana […]
Matendo 20
Paulo Apita Makedonia Na Uyunani 1 Baada ya kumalizika kwa zile ghasia, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawatia moyo, akawaaga, akaanza safari kwenda Makedonia. 2 Alipopita katika sehemu zile, akinena na watu maneno mengi ya kuwatia moyo, ndipo hatimaye akawasili Uyunani, 3 ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa anakaribia kuanza safari kwa njia ya […]
Matendo 21
SAFARI YA TATU YA PAULO YA KITUME Paulo Aenda Yerusalemu 1 Tulipokwisha kujitenga nao, tukaanza safari kwa njia ya bahari moja kwa moja mpaka Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukaenda Patara. 2 Hapo tukapata meli iliyokuwa inavuka kwenda Foinike tukapanda tukasafiri nayo. 3 Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande […]
Matendo 22
Ushuhuda Wa Paulo Kwa Wayahudi Wa Yerusalemu 1 “Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu.” 2 Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakanyamaza kimya kabisa. Ndipo Paulo akasema, 3 “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu, miguuni mwa Gamalieli. Nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, nikiwa mwenye juhudi […]
Matendo 23
1 Paulo akawakazia macho wale wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, nimetimiza wajibu wangu kwa Mungu kwa dhamiri safi kabisa hadi leo.” 2 Kwa ajili ya jambo hili Kuhani Mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi kinywani. 3 Ndipo Paulo akamwambia, “Mungu atakupiga wewe, ewe ukuta uliopakwa chokaa! Wewe umeketi hapo ili […]
Matendo 24
Mbele Ya Feliksi Huko Kaisaria 1 Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania akashuka akiwa amefuatana na baadhi ya wazee pamoja na mwanasheria mmoja aitwaye Tertulo, nao wakaleta mashtaka yao dhidi ya Paulo mbele ya mtawala. 2 Paulo alipoitwa aingie ndani, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akisema, “Mtukufu Feliksi, kwa muda mrefu tumefurahia amani na matengenezo […]
Matendo 25
Paulo Mbele Ya Festo 1 Siku tatu baada ya Festo kuwasili Kaisaria kuchukua wajibu wake mpya, alipanda kwenda Yerusalemu, 2 ambako viongozi wa makuhani na viongozi wa Wayahudi walikuja mbele yake na kuleta mashtaka yao dhidi ya Paulo. 3 Wakamsihi sana Festo, kama upendeleo kwao, aamuru Paulo ahamishiwe Yerusalemu, kwa kuwa walikuwa wanaandaa kumvizia ili […]
Matendo 26
Paulo Ajitetea Mbele Ya Agripa 1 Ndipo Agripa akamwambia Paulo, “Unayo ruhusa kujitetea.” Hivyo Paulo akawaashiria kwa mkono wake, akaanza kujitetea, akasema: 2 “Mfalme Agripa, najiona kuwa na heri kusimama mbele yako leo ninapojitetea kuhusu mashtaka yote ya Wayahudi, 3 hasa kwa sababu unajua vyema desturi zote za Kiyahudi na ya kuwa wewe unajua kwa […]
Matendo 27
Paulo Asafiri Kwa Njia Ya Bahari Kwenda Rumi 1 Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa njia ya bahari kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa askari mmoja jina lake Juliasi, ambaye alikuwa wa kikosi cha walinzi wa Kaisari Agusto. 2 Tulipanda meli iliyotoka Adramitio, iliyokuwa inakaribia kusafiri kwenda kwenye bandari zilizopo pwani ya Asia, tukaanza safari […]