Luka 19

Zakayo Mtoza Ushuru 1 Yesu akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. 2 Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. 3 Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Yesu ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. […]

Luka 20

Wahoji Kuhusu Mamlaka Ya Yesu 1 Siku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wakamjia. 2 Wakamwuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?” 3 Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. 4 Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa […]

Luka 21

Sadaka Ya Mjane 1 Yesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. 2 Akamwona pia mwanamke mmoja mjane maskini, akiweka humo sarafu mbili za shaba. 3 Yesu akasema, “Amin, amin nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo sadaka kubwa zaidi kuliko wengine wote. 4 Hawa watu wengine wote wametoa […]

Luka 22

Yuda Akubali Kumsaliti Yesu 1 Wakati huu Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia. 2 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu. 3 Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili. 4 Yuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa […]

Luka 23

Yesu Apelekwa Kwa Pilato 1 Kisha umati wote wa watu wakainuka na kumpeleka Yesu kwa Pilato. 2 Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” 3 Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe wasema.” 4 […]

Luka 24

Kufufuka Kwa Yesu 1 Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa na kwenda kaburini. 2 Wakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi, 3 lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu. 4 Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa kama […]

Marko 1

Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji 1 Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele yako, yeye atakayeitengeneza njia yako”: 3 “sauti ya mtu aliaye nyikani. ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake.’ ” 4 Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa […]

Marko 2

Yesu Amponya Mtu Aliyepooza 1 Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba amerudi nyumbani. 2 Hivyo watu wengi wakakusanyika kiasi kwamba hapakubaki nafasi yo yote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno. 3 Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. 4 Kwa kuwa walikuwa hawawezi kumfikisha kwa […]

Marko 3

Yesu Amponya Mtu Mwenye Mkono Uliopooza 1 Yesu akaingia tena ndani ya sinagogi na huko palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza. 2 Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. 3 Yesu akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele.” 4 Kisha Yesu akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku […]

Marko 4

Mfano Wa Mpanzi 1 Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umemkusanyikia na kumzunguka ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo. 2 Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema: 3 “Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. 4 Alipokuwa akipanda, mbegu […]