Marko 5

Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo 1 Wakafika upande wa pili wa bahari wakaingia katika nchi ya Wagerasi. 2 Yesu alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini akakutana naye. 3 Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo, 4 kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa kwa minyororo […]

Marko 6

Nabii Hana Heshima Kwao 1 Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake. 2 Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia wakashangaa. Wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! […]

Marko 7

Kilicho Safi Na Kilicho Najisi 1 Mafarisayo na baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu wakakusanyika mbele ya Yesu. 2 Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani, bila kunawa kama ilivyotakiwa na sheria ya dini ya Wayahudi. 3 Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa […]

Marko 8

Yesu Alisha Watu 4,000 1 Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, 2 “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula. 3 Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao […]

Marko 9

1 Yesu akaendelea kuwaambia, “Amin, amin nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija katika nguvu.” Yesu Ageuka Sura 2 Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. 3 Mavazi yake yakawa […]

Marko 10

Mafundisho Kuhusu Talaka 1 Yesu akaondoka huko akavuka Mto wa Yordani, akaenda sehemu ya Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukamjia tena na kama ilivyokuwa desturi yake akawafundisha. 2 Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumwuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?” 3 Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru nini?” 4 Wakajibu, “Mose aliruhusu kwamba […]

Marko 11

Yesu Aingia Yerusalemu Kwa Shangwe 1 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage na Bethania katika Mlima wa Mizeituni, Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake, 2 akiwaambia, “Nendeni kwenye kijiji kilichoko mbele yenu na mara mwingiapo kijijini, mtakuta mwana punda amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote. Mfungueni, mkamlete hapa. 3 Kama mtu ye yote akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ […]

Marko 12

Mfano Wa Wapangaji Waovu 1 Yesu akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akachimba shimo ndani yake kwa ajili ya shinikizo la kusindika divai, akajenga mnara wa ulinzi. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. 2 Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba akamtuma mtumishi […]

Marko 13

Dalili Za Siku Za Mwisho 1 Wakati Yesu alipokuwa akitoka Hekaluni, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa na majengo haya yalivyo mazuri!” 2 Ndipo Yesu akajibu akasema, “Je, unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, yote yatabomolewa.” 3 Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima […]

Marko 14

Shauri La Kumwua Yesu 1 Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa hila na kumwua, 2 kwa kuwa walisema, “Tusilifanye jambo hili wakati wa Sikukuu, maana watu wanaweza wakafanya ghasia.” Yesu Kupakwa […]