Marko 15

Yesu Mbele Ya Pilato 1 Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.” 3 Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. 4 Pilato akamwuliza tena, “Je, […]

Marko 16

Kufufuka Kwa Yesu 1 Sabato ilipomalizika, Maria Magdalene, Maria mama yake Yakobo na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. 2 Asubuhi na mapema, siku ya kwanza ya juma, mara tu baada ya kuchomoza jua walikwenda kaburini. 3 Njiani wakawa wanaulizana wao kwa wao, “Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe kutoka kwenye ingilio la kaburi?” […]

Mathayo 1

Kumbukumbu Za Ukoo Wa Yesu Kristo 1 Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu: 2 Abrahamu akamzaa Isaki, Isaki akamzaa Yakobo, Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake, 3 Yuda akamzaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, Peresi akamzaa Hesroni, Hesroni akamzaa Aramu, 4 Aramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa […]

Mathayo 2

Wataalamu Wa Nyota Wafika Kumwona Mtoto Yesu 1 Baada ya Yesu kuzaliwa katika mji wa Bethlehemu huko Uyahudi, wakati wa utawala wa Mfalme Herode, wataalamu wa mambo ya nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu 2 wakiuliza, “Yuko wapi huyo aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tumeona nyota yake ikitokea mashariki, nasi tumekuja kumwabudu.” 3 Mfalme Herode […]

Mathayo 3

Yohana Mbatizaji Atayarisha Njia 1 Siku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika Nyika ya Uyahudi, akisema, 2 “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu.” 3 Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema, “Sauti ya mtu aliaye huko nyikani, ‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana, yanyosheni mapito yake.’ ” 4 Basi Yohana […]

Mathayo 4

Kujaribiwa Kwa Yesu 1 Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu kuingia nyikani ili akajaribiwe na ibilisi. 2 Baada ya kufunga siku arobaini mchana na usiku, hatimaye akaona njaa. 3 Mjaribu akamjia na kumwambia, “Kama wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.” 4 Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila […]

Mathayo 5

Sifa Za Aliyebarikiwa 1 Basi Yesu alipoona makutano, alipanda mlimani akaketi chini, nao wanafunzi wake wakamjia. 2 Ndipo akaanza kuwafundisha, akisema: 3 “Heri walio maskini wa roho, maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao. 4 Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa. 5 Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi. 6 Heri wenye njaa na kiu […]

Mathayo 6

Kuwapa Wahitaji 1 “Angalieni msitende wema wenu mbele ya watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 “Hivyo mnapowapa wahitaji, msipige panda mbele yenu kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani, ili wasifiwe na watu. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupokea thawabu yao. 3 Lakini ninyi mtoapo […]

Mathayo 7

Kuwahukumu Wengine 1 “Usihukumu ili usije ukahukumiwa. 2 Kwa maana kwa jinsi ile unavyowahukumu wengine, ndivyo utakavyohukumiwa na kwa kipimo kile utakachotoa ndicho utakachopokea. 3 “Kwa nini unatazama kibanzi kidogo kilichomo kwenye jicho la ndugu yako na wala huoni boriti iliyoko kwenye jicho lako? 4 Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Acha nitoe kibanzi kwenye jicho […]

Mathayo 8

Yesu Amtakasa Mwenye Ukoma 1 Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. 2 Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.” 3 Yesu akanyosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka, takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. 4 Kisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu ye yote. […]