Malaki 1

1 Ujumbe: Neno laBwanakwa Israeli kupitia kwa Malaki. Yakobo Alipendwa, Esau Alichukiwa 2 Bwanaasema, “Nimewapenda ninyi.” “Lakini ninyi mnauliza, ‘Wewe umetupendaje?’ ” Bwanaasema, “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo, 3 lakini nikamchukia Esau, nami nimeifanya milima yake kuwa ukiwa na urithi wake nimewapa mbweha wa jangwani.” 4 Edomu anaweza kusema, “Ingawa […]

Malaki 2

Onyo Kwa Makuhani 1 “Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, Enyi makuhani. 2 Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote. 3 “Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka […]

Malaki 3

1 “Angalieni, nitamtuma mjumbe wangu, atakayeiandaa njia mbele yangu. Ndipo ghafula Bwana mnayemtafuta atakuja hekaluni mwake. Mjumbe wa Agano, ambaye mnamwonea shauku, atakuja,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. 2 Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye […]

Malaki 4

Siku Ya Bwana 1 “Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. 2 Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake. Nanyi mtatoka nje na […]

Zekaria 1

Wito Wa Kumrudia Bwana 1 Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema: 2 “Bwanaaliwakasirikia sana baba zako wa zamani. 3 Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asemaBwanaMwenye […]

Zekaria 2

Maono Ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia 1 Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! 2 Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.” 3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye 4 na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu […]

Zekaria 3

Maono Ya Nne: Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu 1 Kisha akanionyesha Yoshua, Kuhani Mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika waBwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshitaki. 2 Bwanaakamwambia Shetani, “Bwanaakukemee Shetani!Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?” 3 Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa […]

Zekaria 4

Maono Ya Tano: Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni Miwili 1 Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka katika usingizi wake. 2 Akaniuliza, “Unaona nini?” Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta […]

Zekaria 5

Maono Ya Sita: Kitabu Kinachoruka 1 Nikatazama tena: na hapo mbele yangu kulikuwa na kitabu kilichoruka! 2 Akaniuliza, “Unaona nini?” # Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka chenye, urefu wa dhiraa ishirinina upana wa dhiraa kumi.” 3 Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila […]

Zekaria 6

Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita 1 Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! 2 Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 3 la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi […]