Hosea 8

Israeli Kuvuna Kisulisuli 1 “Wekeni tarumbeta midomoni mwenu! Tai yuko juu ya nyumba yaBwana kwa sababu watu wamevunja Agano langu, wameasi dhidi ya sheria yangu. 2 Israeli ananililia, ‘Ee Mungu wetu, tunakukubali!’ 3 Lakini Israeli amekataa lile lililo jema, adui atamfuatia. 4 Wanaweka Wafalme bila idhini yangu, wamechagua wakuu bila kibali changu. Kwa fedha zao […]

Hosea 9

Adhabu Kwa Israeli 1 Usifurahie, Ee Israeli; usishangilie kama mataifa mengine. Kwa kuwa hukuwa mwaminifu kwa Mungu wako; umependa ujira wa kahaba kwenye kila sakafu ya kupuria nafaka. 2 Sakafu za kupuria nafaka na mashinikizo ya kukamulia divai havitalisha watu, divai mpya itawapungukia. 3 Hawataishi katika nchi yaBwana, Efraimu atarudi Misri na atakula chakula kilicho […]

Hosea 10

1 Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada. 2 Moyo wao ni mdanganyifu, nao sasa lazima wachukue hatia yao. Bwanaatabomoa madhabahu zao na kuharibu mawe yao ya ibada. 3 Kisha watasema, “Hatuna mfalme kwa sababu hatukumheshimuBwana. Lakini hata […]

Hosea 11

Upendo Wa Mungu Kwa Israeli 1 “Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda, nilimwita mwanangu kutoka Misri. 2 Lakini kadiri nilivyomwita Israeli, ndivyo walivyokwenda mbali nami. Walitoa dhabihu kwa Mabaali na kufukiza uvumba kwa vinyago. 3 Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea, nikiwashika mikono; lakini hawakutambua kuwa ni mimi niliyewaponya. 4 Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu, […]

Hosea 12

1 Efraimu anajilisha upepo; hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima na kuzidisha uongo na jeuri. Anafanya mkataba na Ashuru na kutuma mafuta ya zeituni Misri. 2 Bwanaanalo shtaka dhidi ya Yuda, atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake. 3 Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake; kama […]

Hosea 13

Hasira Ya Bwana Dhidi Ya Israeli 1 Wakati Efraimu alipozungumza, watu walitetemeka, alikuwa ametukuzwa katika Israeli. Lakini alikuwa na hatia ya kumwabudu Baali naye akafa. 2 Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi; wanajitengenezea sanamu kutokana na fedha yao, vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari, vyote kazi ya fundi stadi. Inasemekana kuhusu hawa watu, “Hutoa dhabihu za binadamu […]

Hosea 14

Toba Ya Kuleta Baraka 1 Rudi, Ee Israeli, kwaBwanaMungu wako. Dhambi zako zimekuwa ndilo anguko lako! 2 Chukueni maneno pamoja nanyi, na mumrudieBwana. Mwambieni: “Samehe dhambi zetu zote na utupokee kwa neema, ili tuweze kutoa matunda yetu kama sadaka za mafahali. 3 Ashuru hawezi kutuokoa, hatutapanda farasi wa vita. Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’ kwa […]

Danieli 1

Mafunzo Ya Danieli Huko Babeli 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja akazingira Yerusalemu kwa jeshi. 2 Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza pamoja na baadhi ya vyombo kutoka katika Hekalu la Mungu. Hivi akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko […]

Danieli 2

Ndoto Ya Nebukadneza 1 Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto, akili yake ikasumbuka na hakuweza kulala. 2 Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme, 3 akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua nami nataka nijue maana yake.” 4 Ndipo wanajimu […]

Danieli 3

Sanamu Ya Dhahabu Na Moto Mkali 1 Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitinina upana wake dhiraa sita, akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la nchi ya Babeli. 2 Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo […]