Danieli 4

Ndoto Ya Nebukadneza Ya Mti 1 Mfalme Nebukadneza, Kwa kabila za watu, mataifa na watu wa kila lugha, wanaoishi katika ulimwengu wote: Amani na mafanikio yawe kwenu! 2 Ni furaha yangu kuwaambia kuhusu ishara ya miujiza na maajabu ambayo Mungu Aliye Juu Sana amenifanyia. 3 Tazama jinsi ishara zake zilivyo kuu, jinsi maajabu yake yalivyo […]

Danieli 5

Maandishi Ukutani 1 Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao. 2 Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake […]

Danieli 6

Danieli Katika Tundu La Simba 1 Ilimpendeza Dario kuteua wakuu 120 kutawala katika ufalme wake wote, 2 pamoja na wasimamizi watatu juu yao, ambao mmoja wao alikuwa Danieli. Wakuu walitoa hesabu kwa hao wasimamizi ili mfalme asipate hasara. 3 Basi Danieli alijidhihirisha mwenyewe, miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee hata mfalme […]

Danieli 7

Ndoto Ya Danieli Ya Wanyama Wanne 1 Katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita katika akili yake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake. 2 Danieli akasema: “Katika maono yangu usiku nilitazama, mbele yangu kulikuwepo na upepo kutoka pande nne za mbinguni […]

Danieli 8

Maono Ya Danieli Ya Kondoo Dume Na Beberu 1 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Mfalme Belshaza, mimi Danieli, nilipata maono, baada ya maono ambayo yalikuwa yamenitokea. 2 Katika maono yangu mimi nilijiona nikiwa ndani ya ngome ya Shushani katika jimbo la Elamu, katika maono nilikuwa kando ya Mto Ulai. 3 Nikatazama juu, hapo […]

Danieli 9

Maombi Ya Danieli 1 Katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake Dario mwana wa Ahusuero (mzaliwa wa Umedi) ambaye alifanywa mtawala juu ya ufalme wa Babeli, 2 katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, mimi Danieli, nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno laBwanaalilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini. 3 […]

Danieli 10

Maono Ya Danieli Kuhusu Mtu 1 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono. 2 Wakati huo, mimi Danieli, nikaomboleza kwa majuma matatu. 3 Sikula chakula kizuri, nyama wala divai havikugusa midomo […]

Danieli 11

1 Nami katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake Dario, Mmedi, nilisimama kumsaidia na kumlinda.) Wafalme Wa Kusini Na Wa Kaskazini 2 “Sasa basi, ninakuambia kweli: Wafalme watatu zaidi watatokea Uajemi, kisha atatokea mfalme wa nne, ambaye atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Wakati atakapokuwa amekwisha kujipatia nguvu kwa utajiri wake, atamchochea kila mmoja dhidi […]

Danieli 12

Nyakati Za Mwisho 1 “Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa. 2 Watu wengi ambao wamelala kwenye mavumbi wataamka, baadhi yao kwa uzima […]

Ezekieli 1

Viumbe Hai Na Utukufu Wa Bwana 1 Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, wakati nilipokuwa miongoni mwa hao waliokuwa uhamishoni kando ya Mto Kebari, mbingu zilifunguka nami nikaona maono ya Mungu. 2 Katika siku ya tano ya mwezi, ilikuwa mwaka wa tano wa kuhamishwa kwa Mfalme Yehayakini, 3 neno […]