Anguko La Yerusalemu 1 Hivi ndivyo Yerusalemu ilivyotwaliwa: Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Sedekia wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alilipeleka jeshi lake lote dhidi ya Yerusalemu na akauzunguka. 2 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia […]
Monthly Archives: July 2017
Yeremia 40
Yeremia Aachiwa Huru 1 Neno likamjia Yeremia kutoka kwaBwanabaada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa kifalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli. 2 Kiongozi wa walinzi alipomwona Yeremia, akamwambia, “BwanaMungu wako aliamuru maafa haya kwa ajili ya mahali hapa. […]
Yeremia 41
1 Katika mwezi wa saba, Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, ambaye alikuwa wa uzao wa kifalme na pia alikuwa mmoja wa maafisa wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mizpa. Walipokuwa wakila pamoja huko, 2 Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye […]
Yeremia 42
Yeremia Ashauri Walionusurika Wasihame Yuda 1 Ndipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea na Yezania mwana wa Hoshaya na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia 2 Yeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombeBwanaMungu wako kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa […]
Yeremia 43
1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote yaBwanaMungu wao, kila kituBwanaalichokuwa amemtuma kuwaambia, 2 Azaria mwana wa Hoshaya na Yohanani mwana wa Karea na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo!BwanaMungu wetu hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ 3 Lakini Baruki mwana wa Neria anakuchochea wewe dhidi yetu ili ututie mikononi mwa […]
Yeremia 44
Maafa Kwa Sababu Ya Ibada Za Sanamu 1 Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote waishio Misri, huko Migdoli, Tahpanhesi na Memfisikatika nchi ya Pathrosi, kusema: 2 “Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu 3 […]
Yeremia 45
Ujumbe Kwa Baruki 1 Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruki mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruki kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule: 2 “Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruki: 3 Ulisema, ‘Ole wangu!Bwanaameongeza huzuni […]
Yeremia 46
Ujumbe Kuhusu Misri 1 Hili ni neno laBwanalililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa: 2 Kuhusu Misri: Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Eufrati na Nebukadneza mfalme wa Babeli katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: 3 “Wekeni tayari […]
Yeremia 47
Ujumbe Kuhusu Wafilisti 1 Hili ndilo neno laBwanalililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza: 2 Hili ndilo asemaloBwana: “Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini, yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana. Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake, miji na wale waishio ndani yake. Watu watapiga kelele; wote waishio katika nchi wataomboleza 3 kwa […]
Yeremia 48
Ujumbe Kuhusu Moabu 1 Kuhusu Moabu: Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wa Nebo, kwa maana utaharibiwa. Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; Misgabu itaaibishwa na kuvunjwa vunjwa. 2 Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake: ‘Njoni na tuangamize taifa lile.’ Wewe nawe, Ee Madmeni, utanyamazishwa; upanga utakufuatia. 3 […]