Isaya 47

Anguko La Babeli 1 “Shuka uketi mavumbini, Ee Bikira Binti Babeli; keti chini pasipo na kiti cha enzi, Ee binti wa Wakaldayo. Hutaitwa tena mwororo wala wa kupendeza. 2 Chukua mawe ya kusagia na usage unga, vua shela yako. Pandisha mavazi yako, ondoa viatu vyako, vuka vijito kwa shida. 3 Uchi wako utafunuliwa na aibu […]

Isaya 48

Israeli Mkaidi 1 “Sikilizeni hili, Ee nyumba ya Yakobo, ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli na mnaotoka katika ukoo wa Yuda, ninyi mnaoapa kwa jina laBwana, mnaomwomba Mungu wa Israeli, lakini si katika kweli au kwa haki; 2 ninyi mnaojiita raia wa mji mtakatifu, na kumtegemea Mungu wa Israeli, BwanaMwenye Nguvu Zote ndilo jina lake: […]

Isaya 49

Mtumishi Wa Bwana 1 Nisikilizeni, Enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwaBwanaaliniita, tangu kuzaliwa kwangu amelitaja jina langu. 2 Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa na kunificha katika podo lake. 3 Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika yeye nitaonyesha […]

Isaya 50

Dhambi Ya Israeli Na Utii Wa Mtumishi 1 Hili ndilo asemaloBwana: “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako ambayo kwayo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani miongoni mwa watu wanaonidai? Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, kwa sababu ya makosa mama yenu aliachwa. 2 Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja? Nilipoita, kwa nini […]

Isaya 51

Wokovu Wa Milele Kwa Sayuni 1 “Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia haki na mnaomtafutaBwana: Tazameni katika mwamba ambako ndiko mlikokatwa na mahali pa kuvunjia mawe ambako ndiko mlikochongwa; 2 mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, ambaye ndiye aliyewazaa. Wakati nilipomwita alikuwa mmoja tu, nami nikambariki na kumfanya kuwa wengi. 3 HakikaBwanaataifariji Sayuni naye atayaangalia kwa huruma magofu […]

Isaya 52

1 Amka, amka, Ee Sayuni, jivike nguvu. Vaa mavazi yako ya fahari, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu. Asiyetahiriwa na aliye najisi hataingia kwako tena. 2 Jikung’ute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, Ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako. Ee Binti Sayuni uliye mateka. 3 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana: “Mliuzwa pasipo malipo, nanyi […]

Isaya 53

1 Ni nani aliyeamini ujumbe wetu na mkono waBwana umefunuliwa kwa nani? 2 Alikua mbele yake kama mche mwororo na kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvuta kwake, hakuwa na cho chote katika kuonekana kwake cha kutufanya tumtamani. 3 Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu, mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso. […]

Isaya 54

Utukufu Wa Baadaye Wa Sayuni 1 “Imba, Ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, ninyi ambao kamwe hamkupata utungu wa kuzaa; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asemaBwana. 2 “Panua mahali pa hema lako, tandaza mapazia ya hema […]

Isaya 55

Mwaliko Kwa Wenye Kiu 1 “Njoni, ninyi nyote wenye kiu, njoni kwenye maji; nanyi ambao hamna fedha, njoni, nunueni na mle! Njoni, nunueni divai na maziwa bila fedha na bila gharama. 2 Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula, na kutaabikia kitu kisichoshibisha? Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri, nazo nafsi zenu […]

Isaya 56

Wokovu Kwa Ajili Ya Wengine 1 Hili ndilo asemaloBwana: “Dumisheni haki na mkatende lile lililo sawa, kwa maana wokovu wangu u karibu na haki yangu itafunuliwa upesi. 2 Amebarikiwa mtu yule atendaye hili, mtu yule alishikaye kwa uthabiti, yeye ashikaye Sabato bila kuinajisi, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.” 3 Usimwache mgeni aambatanaye naBwanaaseme, […]