1 Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa: Neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Shukrani Na Kutiwa Moyo 3 Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, […]
Monthly Archives: July 2017
2 Timotheo 2
Askari Mwema Wa Kristo Yesu 1 Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu. 2 Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vile vile. 3 Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. 4 Hakuna askari ye yote ambaye akiwa […]
2 Timotheo 3
Hatari Za Siku Za Mwisho 1 Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. 2 Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, 3 wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa […]
2 Timotheo 4
Maagizo Ya Mwisho 1 Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu watu walio hai na waliokufa wakati wa kuja kwake na ufalme wake kwamba: 2 Uhubiri Neno, uwe tayari wakati ufaao na wakati usiofaa, karipia, kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri. 3 Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali […]
1 Timotheo 1
1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu tumaini letu. 2 Kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani: Neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Maonyo Dhidi Ya Walimu Wa Uongo 3 Kama nilivyokusihi kuendelea kubaki Efeso, wakati nilipokwenda Makedonia, ili […]
1 Timotheo 2
Maagizo Kuhusu Kuabudu 1 Awali ya yote, nasihi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: 2 kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. 3 Jambo hili ni jema tena linapendeza machoni […]
1 Timotheo 3
Sifa Za Waangalizi 1 Hili ni neno la kuaminiwa, kwamba mtu akitamani kazi ya uangalizi, atamani kazi nzuri. 2 Basi, imempasa mwangalizi awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha, 3 asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha. 4 Lazima aweze kuisimamia […]
1 Timotheo 4
Maagizo Kwa Timotheo 1 Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. 2 Mafundisho kama hayo huja kwa kupitia kwa waongo ambao ni wanafiki hali dhamiri zao zikiungua kwa kuchomwa moto. 3 Wao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, […]
1 Timotheo 5
Maagizo Kuhusu Wajane, Wazee Na Watumwa 1 Usimkemee mzee kwa ukali bali umuonye kama vile angekuwa ni baba yako. Uwatendee vijana kama vile ndugu zako, 2 wanawake wazee uwatendee kama mama zako na wanawake vijana kama dada zako, katika usafi wote. 3 Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli. 4 Kama mjane ana watoto […]
1 Timotheo 6
Watumwa 1 Wale wote walio chini ya kongwa la utumwa inawapasa kuwahesabu mabwana zao kuwa wanastahili heshima yote, ili jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu. 2 Wale watumwa ambao wana mabwana waaminio, haiwapasi kupunguza heshima yao kwa sababu wao ni ndugu, badala yake, wawatumikie hata vizuri zaidi, kwa sababu wale wanaonufaika na huduma yao […]