Barua Ya Tatenai Kwa Dario 1 Ndipo nabii Hagai na nabii Zekaria mzao wa Ido, wakawatolea unabii Wayahudi waliokuwa Yuda na Yerusalemu kwa jina la Mungu wa Israeli, aliyekuwa pamoja nao. 2 Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli na Yeshua mwana wa Yosadaki wakaanza kujenga tena nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Nao manabii wa Mungu walikuwa […]
Monthly Archives: July 2017
Ezra 6
Amri Ya Dario 1 Kisha Mfalme Dario alitoa amri, nao wakafanya uchunguzi katika kumbukumbu zilizohifadhiwa katika hazina huko Babeli. 2 Karatasi moja ndefu ya maandishi ilipatikana huko Ekbatana katika jimbo la Umedi. Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa humo: Kumbukumbu: 3 Katika mwaka wa kwanza wa kutawala Mfalme Koreshi, mfalme alitoa amri kuhusu Hekalu la Mungu katika […]
Ezra 7
Ezra Awasili Yerusalemu 1 Baada ya mambo haya, wakati wa utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Ezra mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia, 2 mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu, 3 mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi, 4 mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa […]
Ezra 8
Orodha Ya Viongozi Wa Jamaa Waliorudi Na Ezra 1 Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta: 2 wa wazao wa Finehasi, alikuwa Gershoni; wa wazao wa Ithamari, alikuwa Danieli; wa wazao wa Daudi, alikuwa Hatushi 3 wa wazao wa Shekania; wa […]
Ezra 9
Maombi Ya Ezra Kuhusu Kuoa Wake Wa Kigeni 1 Baada ya mambo haya kutendeka, viongozi walinijia na kusema, “Watu wa Israeli, wakiwemo makuhani na Walawi, hawakujitenga na majirani zao katika kufanya machukizo, kama yale ya Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Waamoni, Wamoabi, Wamisri na Waamori. 2 Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake […]
Ezra 10
Toba Ya Watu 1 Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana. 2 Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake […]
2 Mambo ya nyakati 1
Solomoni Aomba Hekima 1 Solomoni mwana wa Daudi alijiimarisha kwenye milango yote! Katika ufalme wake, kwa kuwaBwanaMungu wake alikuwa pamoja naye, naye akamfanya mkuu mno. 2 Ndipo Solomoni akasema na Israeli wote, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, waamuzi na viongozi wote katika Israeli, pamoja na wakuu wa jamaa. 3 Naye Solomoni na kusanyiko […]
2 Mambo ya nyakati 2
Maandalizi Ya Kujenga Hekalu 1 Solomoni akatoa amri kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina laBwanana jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe. 2 Akaandika watu 70,000 kuwa wachukuzi wa mizigo, na watu 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na watu 3,600 kuwa wasimamizi wao. 3 Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: “Unitumie magogo […]
2 Mambo ya nyakati 3
Solomoni Ajenga Hekalu 1 Ndipo Solomoni akaanza kujenga Hekalu laBwanakatika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapoBwanaalikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi. 2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. 3 Msingi aliouweka Solomoni kwa […]
2 Mambo ya nyakati 4
Vifaa Vya Hekalu 1 Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini, upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi. 2 Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kina chake kilikuwa dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathiniingeweza kuizunguka. 3 Chini […]