2 Wafalme 20

Ugonjwa Wa Hezekia 1 Katika siku zile, Hezekia akaugua na akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea na kusema, “Hivi ndivyoBwanaasemavyo: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.” 2 Hezekia akaelekeza uso wake ukutani akamwombaBwanaakisema, 3 “EeBwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na […]

2 Wafalme 21

Manase Mfalme Wa Yuda 1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka hamsini na mitano. Jina la mama yake aliitwa Hefsiba. 2 Akafanya maovu machoni paBwana, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayoBwanaaliyafukuza mbele ya Waisraeli. 3 Akajenga tena mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo […]

2 Wafalme 22

Kitabu Cha Torati Chapatikana 1 Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi. 2 Akafanya yaliyo mema machoni paBwanana kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake, bila kugeuka upande wa kuume wala wa kushoto. 3 Katika mwaka […]

2 Wafalme 23

Yosia Analifanya Upya Agano 1 Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu. 2 Akapanda mpaka kwenye Hekalu laBwanapamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote kuanzia aliye mdogo hadi aliye mkubwa kabisa. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu laBwana. […]

2 Wafalme 24

1 Wakati wa utawala wa Yehoiakimu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliishambulia nchi, naye Yehoiakimu akawa mtumwa wake kwa miaka mitatu. Lakini hatimaye akabadili mawazo yake na kuasi dhidi ya Nebukadneza. 2 Bwanaakatuma Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia ghafula. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno laBwanalililosemwa na watumishi wake manabii. 3 Hakika mambo haya […]

1 Wafalme 1

Adonia Ajitangaza Mwenyewe Kuwa Mfalme 1 Mfalme Daudi alipokuwa mzee umri ukiwa umesogea, hakuweza kupata joto hata walipomfunika kwa nguo. 2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Turuhusu tumtafute kijana mwanamwali bikira amhudumie mfalme na kumtunza. Anaweza kulala pembeni mwake ili bwana wetu mfalme apate joto.” 3 Kisha wakatafuta katika Israeli yote ili kumpata msichana mzuri […]

1 Wafalme 2

Maagizo Ya Daudi Kwa Solomoni 1 Siku zilipokaribia za Daudi kufa, akampa mwanawe Solomoni agizo. 2 Akasema, “Mimi ninakaribia kwenda njia ya dunia yote. Hivyo uwe hodari, jionyeshe kuwa mwanaume, 3 shika lileBwanaMungu wako analokuagiza: Enenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, […]

1 Wafalme 3

Solomoni Anaomba Hekima 1 Solomoni akafanya urafiki na Mfalme Farao wa Misri na kumwoa binti yake. Akamleta huyo binti katika Mji wa Daudi mpaka alipomaliza kujenga jumba lake la kifalme na Hekalu laBwana, pamoja na ukuta kuzunguka Yerusalemu. 2 Hata hivyo, watu bado walikuwa wakitoa dhabihu huko kwenye vilima, kwa sababu Hekalu lilikuwa bado halijajengwa […]

1 Wafalme 4

Maafisa Wa Solomoni Na Watawala 1 Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote. 2 Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu: Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki; 3 Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani; 4 Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi; Sadoki na Abiathari: makuhani; 5 Azaria mwana wa Nathani: […]