1 Wafalme 5

Maandalio Ya Ujenzi Wa Hekalu 1 Hiramu mfalme wa Tiro aliposikia kuwa Solomoni ametiwa mafuta awe mfalme mahali pa Daudi baba yake, akatuma wajumbe kwa Solomoni, kwa sababu Hiramu siku zote alikuwa na uhusiano mzuri wa kirafiki na Daudi. 2 Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu: 3 “Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi […]

1 Wafalme 6

Solomoni Ajenga Hekalu 1 Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu laBwana. 2 Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili yaBwanalilikuwa na urefu wa dhiraa sitini, upana wa […]

1 Wafalme 7

Solomoni Ajenga Jumba Lake La Kifalme 1 Ilimchukua Solomoni miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. 2 Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini, likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi […]

1 Wafalme 8

Sanduku La Agano Laletwa Hekaluni 1 Kisha Mfalme Solomoni akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano laBwanakutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 2 Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa Mfalme Solomoni wakati wa sikukuu ya mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi […]

1 Wafalme 9

Bwana Anamtokea Solomoni 1 Solomoni alipomaliza kujenga Hekalu laBwanapamoja na jumba la kifalme, alipokwisha kufanya yote aliyotaka kufanya, 2 Bwanaakamtokea mara ya pili, kama alivyokuwa amemtokea huko Gibeoni. 3 Bwanaakamwambia: “Nimesikia dua na maombi uliyofanya mbele zangu, nimeliweka wakfu Hekalu hili ambalo umelijenga, kwa kuweka Jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwa […]

1 Wafalme 10

Malkia Wa Sheba Amtembelea Solomoni 1 Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni na uhusiano wake na jina laBwana, malkia alikuja kumjaribu kwa maswali magumu. 2 Alipofika Yerusalemu pamoja na msafara mkubwa sana: pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani; alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu […]

1 Wafalme 11

Wakeze Solomoni 1 Hata hivyo, Mfalme Solomoni akawapenda wanawake wengi wa kigeni zaidi, mbali na binti Farao: wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti. 2 Wakitoka katika mataifa ambayoBwanaaliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Solomoni akakaza kuwapenda. 3 Alikuwa na wake 700 wa uzao wa […]

1 Wafalme 12

Israeli Yaasi Dhidi Ya Rehoboamu 1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wamekwenda huko kumfanya yeye kuwa mfalme. 2 Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Solomoni), akarudi kutoka Misri. 3 Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu, yeye na kusanyiko lote la Israeli wakamwendea […]

1 Wafalme 13

Mtu Wa Mungu Kutoka Yuda 1 Kwa neno laBwana, mtu wa Mungu alifika Betheli kutoka Yuda wakati Yeroboamu alipokuwa amesimama kando ya madhabahu ili kutoa sadaka. 2 Akapiga kelele dhidi ya madhabahu kwa neno laBwana: “Ee madhabahu, madhabahu! Hivi ndivyo asemavyoBwana: ‘Mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika nyumba ya Daudi. Juu yako atawatoa dhabihu makuhani wa […]

1 Wafalme 14

Unabii Wa Ahiya Dhidi Ya Yeroboamu 1 Wakati ule Abiya mwana wa Yeroboamu akaugua, 2 naye Yeroboamu akamwambia mke wake, “Nenda ukajibadilishe, ili watu wasijue kwamba wewe ni mke wa Yeroboamu. Kisha uende Shilo. Nabii Ahiya yuko huko, yule aliyeniambia kuwa nitakuwa mfalme juu ya watu hawa. 3 Chukua mikate kumi, maandazi kadhaa na gudulia […]