Abiya Mfalme Wa Yuda 1 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda, 2 naye akatawala katika Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu. 3 Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwaBwanaMungu wake kama moyo wa Daudi […]
Monthly Archives: July 2017
1 Wafalme 16
1 Ndipo neno laBwanalikamjia Yehu mwana wa Hanani dhidi ya Baasha, kusema: 2 “Nilikuinua kutoka mavumbini na kukufanya kiongozi wa watu wangu Israeli, lakini ukaenenda katika njia za Yeroboamu na kusababisha watu wangu Israeli kutenda dhambi na kunikasirisha kwa dhambi zao. 3 Basi nitamwangamiza Baasha pamoja na nyumba yake, nami nitaifanya nyumba yako kama ile […]
1 Wafalme 17
Eliya Analishwa Na Kunguru 1 Basi Eliya, Mtishbi kutoka Tishbi katika Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye ninamtumikia, hapatakuwa na umande wala mvua katika miaka hii isipokuwa kwa neno langu.” 2 Kisha neno laBwanalikamjia Eliya, kusema, 3 “Ondoka hapa, elekea upande wa mashariki ukajifiche katika Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani. 4 […]
1 Wafalme 18
Eliya Na Obadia 1 Baada ya muda mrefu, katika mwaka wa tatu, neno laBwanalikamjia Eliya kusema, “Nenda ukajionyeshe kwa Ahabu na mimi nitanyesha mvua juu ya nchi.” 2 Kwa hiyo Eliya akaenda kujionyesha kwa Ahabu. Wakati huu njaa ilikuwa kali sana katika Samaria, 3 naye Ahabu alikuwa amemwita Obadia ambaye alikuwa msimamizi wa jumba lake […]
1 Wafalme 19
Eliya Akimbilia Horebu 1 Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Eliya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 2 Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Hao miungu initendee hivyo na kuzidi, kama kufikia kesho wakati kama huu sitaifanya roho yako kama mmojawapo wa hao manabii.” 3 Eliya aliogopa, na akakimbia kuokoa maisha yake. […]
1 Wafalme 20
Ben-Hadadi Aishambulia Samaria 1 Wakati huu, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote. Akifuatana na wafalme thelathini na wawili wakiwa na farasi na magari ya vita, akakwea kuuzingira kwa jeshi Samaria na kuishambulia. 2 Akawatuma wajumbe katika mji kwa Ahabu mfalme wa Israeli, kusema, “Hivi ndivyo asemavyo Ben-Hadadi: 3 ‘Fedha yako na dhahabu ni […]
1 Wafalme 21
Shamba La Mizabibu La Nabothi 1 Baada ya hayo, Nabothi, Myezreeli, alikuwa na shamba la mizabibu jirani na jumba la kifalme la Ahabu mfalme wa Samaria. 2 Ahabu akamwambia Nabothi, “Unipatie shamba lako la mizabibu nilitumie kwa bustani ya mboga, kwa kuwa liko karibu na jumba langu la kifalme. Badala yake, nitakupa shamba jingine la […]
1 Wafalme 22
Mikaya Anatabiri Dhidi Ya Ahabu 1 Kwa miaka mitatu hapakuwa na vita kati ya Aramu na Israeli. 2 Lakini katika mwaka wa tatu Yehoshafati mfalme wa Yuda akashuka kwenda kumwona mfalme wa Israeli. 3 Mfalme wa Israeli alikuwa amewaambia maafisa wake, “Je, hamjui Ramoth-Gileadi ni mali yetu na bado hatufanyi cho chote kuirudisha kwetu kutoka […]
2 Samweli 1
Daudi Afahamishwa Kifo Cha Sauli 1 Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alipokuwa amerudi kutoka kuwashinda Waamaleki, Daudi alikaa siku mbili huko Siklagi. 2 Siku ya tatu akaja mtu mwenye nguo zilizoraruka na mavumbi kichwani mwake kutoka kwenye kambi ya Sauli. Alipomjia Daudi, akajitupa chini ili kumpa heshima. 3 Daudi akamwuliza, “Wewe umetoka wapi?” Akamjibu, […]
2 Samweli 2
Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Yuda 1 Ikawa baada ya mambo haya, Daudi akamwulizaBwana, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?” Bwanaakasema, “Panda.” Daudi akauliza, “Je, niende wapi?” Bwanaakajibu, “Nenda Hebroni.” 2 Basi Daudi akakwea kwenda huko pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. […]