2 Samweli 3

1 Vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi vilidumu kwa muda mrefu. Daudi akaendelea kuwa imara zaidi na zaidi, wakati nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika zaidi na zaidi. 2 Wana walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni: Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni, mwana wa Ahinoamu wa Yezreeli; 3 mzaliwa wake wa pili alikuwa […]

2 Samweli 4

Ish-Boshethi Anauawa 1 Ish-Boshethi mwana wa Sauli aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, akakosa ujasiri, nayo Israeli yote wakatiwa hofu kuu. 2 Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili ambao walikuwa viongozi wa vikundi vya uvamizi. Mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu, waliokuwa wana wa Rimoni, Mbeerothi, kutoka kabila la Benyamini. Beerothi alihesabiwa kuwa […]

2 Samweli 5

Daudi Awa Mfalme Juu Ya Israeli 1 Makabila yote ya Israeli yakamjia Daudi huko Hebroni na kumwambia, “Sisi tu nyama yako na damu yako hasa. 2 Zamani, wakati Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ulikuwa ndiye uliyeongoza Israeli vitani. NayeBwanaakakuambia, ‘Utawachunga watu wangu Israeli, nawe utakuwa kiongozi wao.’ ” 3 Wazee wote wa Israeli wakamwendea […]

2 Samweli 6

Sanduku La Mungu Laletwa Yerusalemu 1 Daudi akakusanya tena watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa. 2 Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yudakuleta kutoka huko Sanduku la Mungu, linaloitwa kwa Jina, naam, jina laBwanaMwenye Nguvu Zote, ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku. 3 Wakaweka hilo Sanduku […]

2 Samweli 7

Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi 1 Baada ya mfalme kukaa katika jumba lake la kifalme kwa utulivu, nayeBwanaakiwa amemstarehesha pande zote mbali na adui zake, 2 akamwambia nabii Nathani, “Mimi hapa, ninaishi katika jumba la kifalme la mierezi, wakati Sanduku la Mungu limebaki katika hema.” 3 Nathani akamjibu mfalme, “Lo lote ulilo nalo moyoni, endelea […]

2 Samweli 8

Ushindi Wa Daudi 1 Ikawa baada ya jambo hili, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, akateka Metheg-Amma kutoka mikononi mwa Wafilisti. 2 Pia Daudi akawashinda Wamoabu. Akawafanya walale chini kwa mstari akawapima kwa urefu wa kamba. Kila alipopima urefu wa hiyo kamba mara mbili hilo kundi waliuawa na alipopima mara ya tatu aliwaacha hai. Kwa hiyo […]

2 Samweli 9

Daudi Na Mefiboshethi 1 Daudi akauliza, “Je, hakuna mtu hata mmoja wa nyumba ya Sauli aliyebaki ambaye naweza kumtendea wema kwa ajili ya Yonathani?” 2 Basi palikuwepo mtumishi wa nyumba ya Sauli aliyeitwa Siba. Wakamwita aje mbele ya Daudi, naye mfalme akamwambia, “Wewe ndiwe Siba?” Akamjibu, “Naam, mimi ndiye mtumishi wako.” 3 Mfalme akauliza, “Je, […]

2 Samweli 10

Daudi Awashinda Waamoni 1 Baada ya muda, mfalme wa Waamoni akafa, naye Hanuni mwanawe akaingia mahali pake. 2 Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kama vile baba yake alivyonitendea mimi wema.” Hivyo Daudi akatuma ujumbe kuonyesha wema wake kwa Hanuni kuhusu baba yake. Watu wa Daudi walipofika katika nchi ya Waamoni, 3 wakuu […]

2 Samweli 11

Daudi Na Bathsheba 1 Katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati wafalme watokapo kwenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu pamoja na watu wa mfalme na jeshi lote la Israeli. Wakawaangamiza Waamoni na kuuzunguka kwa jeshi mji wa Raba. Lakini Daudi akabaki Yerusalemu. 2 Ikawa siku moja wakati wa jioni Daudi aliinuka kitandani mwake na kutembeatembea juu ya […]

2 Samweli 12

Nathani Amkemea Daudi 1 Bwanaakamtuma Nathani kwa Daudi. Alipofika kwake akamwambia, “Katika mji mmoja kulikuwapo na watu wawili, mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini. 2 Yule mtu tajiri alikuwa na idadi kubwa sana ya kondoo na ng’ombe, 3 lakini yule maskini hakuwa na cho chote ila kondoo jike mdogo aliyekuwa amemnunua. Akamtunza kondoo huyo, […]