Amnoni Na Tamari 1 Ikawa baada ya hayo, Amnoni mwana wa Daudi akampenda Tamari, umbu lake Absalomu mwana wa Daudi, ambaye alikuwa mzuri wa sura. 2 Amnoni akasumbuka sana kuhusu Tamari hata akaugua, kwa kuwa Tamari alikuwa bikira, na ilionekana kwamba haiwezekani Amnoni kumfanyia jambo lo lote. 3 Basi Amnoni alikuwa na rafiki jina lake […]
Monthly Archives: July 2017
2 Samweli 14
Absalomu Arudi Yerusalemu 1 Yoabu mwana wa Seruya akafahamu kuwa moyo wa mfalme ulikuwa na shauku ya kumwona Absalomu. 2 Kwa hiyo Yoabu akamtuma mtu fulani kwenda Tekoa na kumleta mwanamke mwenye hekima kutoka huko. Akamwambia huyo mwanamke, “Jifanye uko katika maombolezo. Vaa nguo za kuomboleza, nawe usitumie mafuta yo yote ya uzuri, jifanye kama […]
2 Samweli 15
Mipango Ya Hila Ya Absalomu 1 Baada ya muda, Absalomu akajipatia magari ya vita na farasi pamoja na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake. 2 Akawa anaamka asubuhi na mapema na kusimama kando ya barabara inayoelekea kwenye lango la mji. Wakati wo wote alipokuja mtu ye yote mwenye mashtaka yanayohitaji kuletwa mbele ya mfalme […]
2 Samweli 16
Daudi Na Siba 1 Daudi alipokuwa amekwenda umbali mfupi kupita kilele cha mlima, akamkuta huko Siba, msimamizi wa shughuli za Mefiboshethi, akingojea kumlaki Daudi. Alikuwa na punda wawili wakiwa wametandikwa na kupakiwa mikate mia mbili, maandazi mia ya zabibu kavu, maandazi mia ya tini na kiriba cha divai. 2 Mfalme Daudi akamwuliza Siba, “Kwa nini […]
2 Samweli 17
1 Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Nipe ruhusa niwachague watu kumi na mbili elfu na waanze safari usiku huu huu kumfuatia Daudi. 2 Nitamshambulia wakati akiwa amechoka na ni dhaifu. Nitampiga na hofu, na kisha watu wote walio pamoja naye watakimbia. Nitampiga mfalme peke yake 3 na kuwarudisha watu wote kwako. Kifo cha mtu yule unayemtafuta kitamaanisha […]
2 Samweli 18
Kifo Cha Absalomu 1 Daudi akakusanya watu aliokuwa nao na kuweka majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia. 2 Daudi akatuma vikosi vya askari: theluthi moja ilikuwa chini ya amri ya Yoabu, theluthi ya pili chini ya Abishai mwana wa Seruya nduguye Yoabu, na theluthi ya tatu chini ya Itai, Mgiti. Mfalme akaviambia vikosi, “Hakika […]
2 Samweli 19
Yoabu Amkemea Mfalme 1 Yoabu akaambiwa, “Mfalme analia na kumwombolezea Absalomu.” 2 Kwa jeshi lote, ushindi wa siku ile ukageuka kuwa maombolezo, kwa sababu siku ile vikosi vilisikia ikisemwa, “Mfalme anahuzunika kwa ajili ya mwanawe.” 3 Siku ile watu wakaingia mjini kimya kama vile waingiavyo kwa aibu watu waliokimbia kutoka vitani. 4 Mfalme akafunika uso […]
2 Samweli 20
Sheba Aasi Dhidi Ya Daudi 1 Basi, kulikuwa na mtu mbaya sana aliyeitwa Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini, aliyekuwako huko. Akapiga tarumbeta na kupaza sauti, “Hatuna fungu katika Daudi, wala hatuna sehemu katika mwana wa Yese! Kila mtu aende hemani mwake, Enyi Israeli!” 2 Kwa hiyo watu wote wa Israeli wakamwacha Daudi na kumfuata Sheba […]
2 Samweli 21
Wagibeoni Wanalipiza Kisasi 1 Wakati wa utawala wa Daudi kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu mfululizo, kwa hiyo Daudi akautafuta uso waBwana.Bwanaakasema, “Ni kwa sababu ya Sauli na nyumba yake iliyotiwa madoa ya damu, kwa sababu aliwaua Wagibeoni.” 2 Mfalme akawaita Wagibeoni na kuzumgumza nao. (Wagibeoni hawakuwa wa wana wa Israeli, ila walikuwa mabaki ya […]
2 Samweli 22
Wimbo Wa Daudi Wa Sifa 1 Daudi akamwimbiaBwanamaneno ya wimbo huu hapoBwanaalipomwokoa kutoka katika mkono wa adui zake wote, pia kutoka katika mkono wa Sauli. 2 Akasema: “Bwanani mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, 3 Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake nakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, […]