Sauli Ajaribu Kumwua Daudi 1 Sauli akamwambia mwanawe Yonathani na watumishi wake wote wamwue Daudi. Lakini Yonathani mwana wa Sauli alimpenda sana Daudi, 2 naye akamwonya, akisema, “Baba yangu Sauli anatafuta nafasi ya kukuua. Ujilinde kesho asubuhi, nenda ukajifiche na ukae huko. 3 Nitatoka na kukaa na baba yangu shambani mahali uliko. Nitazungumza naye juu […]
Monthly Archives: July 2017
1 Samweli 20
Daudi Na Yonathani 1 Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akamwendea Yonathani na kumwuliza, “Kwani nimefanya nini? Kosa langu ni nini? Nimemkosea baba yako kwa jinsi gani, hata kwamba anajaribu kuuondoa uhai wangu?” 2 Yonathani akajibu, “La hasha! Hutakufa! Tazama, baba yangu hafanyi kitu cho chote, kikubwa au kidogo, bila kuniambia mimi. Kwa nini […]
1 Samweli 21
Daudi Huko Nobu 1 Daudi akaenda Nobu, kwa Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akatetemeka alipokutana naye, akamwuliza, “Kwa nini uko peke yako? Kwa nini hukufuatana na mtu ye yote?” 2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, “Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu ye yote asijue cho chote kuhusu kazi yake wala maagizo yako!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia […]
1 Samweli 22
Daudi Akiwa Adulamu Na Mispa 1 Daudi akaondoka Gathi na kukimbilia kwenye pango la Adulamu. Ndugu zake na watu wa nyumba ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. 2 Wale wote waliokuwa katika dhiki au waliokuwa na madeni au wale ambao hawakuridhika wakamkusanyikia Daudi, naye akawa kiongozi wao. Watu wapatao 400 walikuwa pamoja naye. […]
1 Samweli 23
Daudi Aokoa Keila 1 Daudi alipoambiwa kuwa, “Tazama, Wafilisti wanapigana dhidi ya Keila nao wanapokonya nafaka katika sakafu za kupuria,” 2 akauliza kwaBwana, akisema, “Je, niende na kuwashambulia hawa Wafilisti?” Bwanaakamjibu, “Nenda, washambulie Wafilisti na uiokoe Keila.” 3 Lakini watu wa Daudi wakamwambia, “Hapa Yuda kwenyewe tunaogopa. Si zaidi sana, kama tukienda Keila dhidi ya […]
1 Samweli 24
Daudi Amwacha Sauli Hai 1 Baada ya Sauli kurudi kuwafuatia Wafilisti, akaambiwa kwamba, “Daudi yuko katika Jangwa la En-Gedi.” 2 Basi Sauli akachukua watu hodari 3,000 kutoka Israeli yote kwenda kumsaka Daudi na watu wake karibu na Majabali ya Mbuzi Mwitu. 3 Akaja mpaka kwenye mazizi ya kondoo kando ya njia, hapo palikuwa na pango, […]
1 Samweli 25
Daudi, Nabali Na Abigaili 1 Basi Samweli akafa, nao Israeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akatelemka kwenye Jangwa la Maoni. 2 Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na mali huko Karmeli, yeye alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli. 3 […]
1 Samweli 26
Daudi Amwacha Sauli Hai Tena 1 Hao Wazifu wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kinachotazamana na Yeshimoni?” 2 Hivyo Sauli akashuka kwenda katika Jangwa la Zifu, akiwa na watu wake 3,000 wa Israeli waliochaguliwa, kumsaka Daudi huko. 3 Sauli akapiga kambi yake kando ya barabara juu ya kilima […]
1 Samweli 27
Daudi Miongoni Mwa Wafilisti 1 Daudi akasema moyoni mwake, “Katika mojawapo ya siku hizi nitaangamizwa kwa mkono wa Sauli. Jambo lililo bora ni kutorokea kwenye nchi ya Wafilisti. Hivyo Sauli atakata tamaa ya kunisaka po pote katika Israeli, nami nitakuwa nimeponyoka mkononi mwake.” 2 Hivyo Daudi akaondoka na hao watu mia sita waliokuwa pamoja naye […]
1 Samweli 28
Sauli Na Mchawi Wa Endori 1 Siku zile Wafilisti wakakusanya majeshi yao ili kupigana vita dhidi ya Israeli. Akishi akamwambia Daudi, “Lazima ujue kuwa wewe pamoja na watu wako mtafuatana nami kwenda vitani.” 2 Daudi akasema, “Ndipo wewe mwenyewe utakapojionea jambo ambalo mtumishi wako anaweza kufanya.” Akishi akamjibu Daudi, “Vyema sana, mimi nitakufanya uwe mlinzi […]