Akishi Amrudisha Daudi Huko Siklagi 1 Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki, nao Waisraeli wakapiga kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli. 2 Watawala wa Wafilisti walipokuwa wakipita pamoja na vikosi vyao vya mamia na vya maelfu, Daudi na watu wake walikuwa wakitembea huko nyuma pamoja na Akishi. 3 Majemadari wa Wafilisti wakauliza, “Vipi kuhusu […]
Monthly Archives: July 2017
1 Samweli 30
Daudi Aangamiza Waamaleki 1 Daudi na watu wake wakafika Siklagi siku ya tatu. Basi Waamaleki walikuwa wamevamia Negebu na Siklagi. Wakawa wameshambulia mji wa Siklagi na kuuteketeza kwa moto, 2 nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakuua ye yote, bali waliwachukua wakaenda zao. 3 Daudi na watu wake […]
1 Samweli 31
Sauli Ajiua 1 Basi Wafilisti wakapigana dhidi ya Israeli. Waisraeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, na wengi wakauawa kwenye Mlima wa Gilboa. 2 Wafilisti wakawasonga Sauli na wanawe kwa nguvu, na kuwaua wanawe Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. 3 Mapigano yakawa makali sana kumzunguka Sauli, nao wapiga upinde wakampata na kumjeruhi vibaya. 4 Sauli akamwambia mchukua silaha […]
Ruthu 1
Naomi Na Ruthu 1 Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi, akaondoka mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu. 2 Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu […]
Ruthu 2
Ruthu Akutana Na Boazi 1 Basi Naomi alikuwa na jamaa wa upande wa mume wake, kutoka katika ukoo wa Elimeleki, jina lake aliitwa Boazi. 2 Ruthu, Mmoabi, akamwambia Naomi, “Nitakwenda mashambani nikaokote mabaki ya nafaka nyuma ya yule nitakayepata kibali machoni pake.” Naomi akamwambia, “Nenda, binti yangu.” 3 Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka nyuma […]
Ruthu 3
Ruthu Na Boazi Kwenye Sakafu Ya Kupuria 1 Kisha Naomi akamwambia mkwewe, “Binti yangu, je, nisingelikutafutia pumziko ambako utatunzika vyema? 2 Je, Boazi, ambaye umekuwa pamoja na watumishi wake wasichana, si jamaa yetu wa karibu? Usiku wa leo atakuwa anapepeta ngano kwenye sakafu ya kupuria. 3 Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie nguo zako nzuri. […]
Ruthu 4
Boazi Amwoa Ruthu 1 Boazi akakwea mpaka kwenye lango la mji, akaketi pale. Kisha muda si mrefu yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, “Njoo hapa rafiki yangu, karibu uketi.” Naye akakaribia, akaketi. 2 Boazi akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, “Ketini hapa.” Nao […]
Waamuzi 1
Israeli Wapigana Na Wakanaani Waliobaki 1 Baada ya kifo cha Yoshua, Waisraeli wakamwulizaBwana, “Ni nani atakayetangulia kupanda mbele yetu kwa ajili ya kupigana na Wakanaani?” 2 Bwanaakajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia; nimewapa hiyo nchi mikononi mwao.” 3 Ndipo watu wa Yuda wakawaambia Wasimeoni ndugu zao, “Pandeni pamoja nasi katika nchi tuliyopewa, ili tupate kupigana na Wakanaani. […]
Waamuzi 2
Malaika Wa Bwana Huko Bokimu 1 Malaika waBwanaakakwea kutoka Gilgali hadi Bokimu, naye akasema, “Niliwapandisha kutoka Misri na kuwaingiza katika nchi niliyoapa kuwapa baba zenu. Nikasema, ‘Kamwe sitalivunja Agano langu nanyi. 2 Nanyi msifanye agano na watu wa nchi hii, bali mtazibomoa madhabahu zao.’ Lakini ninyi hamkunitii mimi. Kwa nini mmefanya jambo hili? 3 Sasa […]
Waamuzi 3
Mataifa Yaliyobaki Katika Ile Nchi 1 Haya ndiyo mataifaBwanaaliyoyaacha ili kuwajaribu Waisraeli wote ambao hawakujua vita yo yote ya Kanaani 2 (alifanya hivi ili tu kuwafundisha wazao wa Waisraeli ambao hawakuwa wamejua vita hapo awali): 3 wafalme watano wa Wafilisti, Wakanaani wote, Wasidoni, Wahivi waishio katika milima ya Lebanoni kuanzia Mlima wa Baal-Hermoni hadi Lebo-Hamathi. […]