Waamuzi 4

Debora 1 Baada ya Ehudi kufa, Waisraeli wakafanya tena maovu machoni paBwana. 2 HivyoBwanaakawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Jemadari wa jeshi lake alikuwa Sisera, aliyeishi huko Haroshethi-Hagoyimu. 3 Kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma yapatayo 900, naye alikuwa amewatesa Waisraeli kwa ukatili kwa muda wa miaka ishirini, Waisraeli […]

Waamuzi 5

Wimbo Wa Debora 1 Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu: 2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza, wakati watu wanapojitoa kwa hiari yao wenyewe: mhimidiniBwana! 3 “Sikieni hili, enyi wafalme! Sikilizeni, enyi watawala! NitamwimbiaBwana, nitaimba; kwa wimbo nitamhimidiBwana, Mungu wa Israeli. 4 “EeBwana, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, […]

Waamuzi 6

Gideoni 1 Waisraeli wakafanya tena yaliyo maovu mbele zaBwana, naye kwa miaka sabaBwanaakawatia mikononi mwa Wamidiani. 2 Mkono wa Midiani ukawa na nguvu dhidi ya Israeli na kwa ajili ya Wamidiani, Waisraeli wakajitengenezea mahali pa kujificha milimani, kwenye mapango na ngome. 3 Kila wakati Waisraeli walipopanda mazao mashambani, Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki […]

Waamuzi 7

Gideoni Awashinda Wamidiani 1 Ndipo Yerub-Baali (yaani Gideoni) na lile jeshi lililokuwa pamoja naye, wakaondoka asubuhi na mapema na kupiga kambi kando ya chemchemi ya Harodi. Kambi ya Wamidiani ilikuwa kaskazini yao katika bonde karibu na kilima cha More. 2 Bwanaakamwambia Gideoni, “Jeshi lililo pamoja nawe ni kubwa sana kwa mimi kuwatia Wamidiani mikononi mwao. […]

Waamuzi 8

Ushindi Wa Gideoni Na Kulipiza Kisasi 1 Basi Waifraimu wakamwuliza Gideoni, “Mbona mmetutenda hivi? Kwa nini hukutuita ulipokwenda kupigana na Wamidiani?” Wakawalaumu kwa ukali sana. 2 Gideoni akawajibu, “Nilichofanya mimi ni nini kulinganisha na kile ninyi mlichofanya? Je, kuokoa masazo ya zabibu za Efraimu si bora kuliko mavuno kamili ya zabibu ya Abiezeri? 3 Mungu […]

Waamuzi 9

Abimeleki Ajaribu Kuanzisha Ufalme 1 Siku moja Abimeleki mwana wa Yerub-Baali akaenda kwa ndugu wa mama yake huko Shekemu na kuwaambia yeye na ukoo wote wa mama yake, 2 “Waulizeni watu wote wa Shekemu, ‘Lipi lililo bora kwenu: Kutawaliwa na wana wote sabini wa Yerub-Baali, au mtu mmoja peke yake?’ Kumbukeni kwamba, mimi ni mfupa […]

Waamuzi 10

Tola 1 Baada ya Abimeleki, Tola mwana wa Pua mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, aliyeishi huko Shamiri, katika nchi ya vilima ya Efraimu, akainuka kuokoa Israeli. 2 Akaamua Israeli kwa miaka ishirini na mitatu. Ndipo akafa, naye akazikwa huko Shamiri. Yairi 3 Baada yake akafuatiwa na Yairi, Mgileadi, ambaye aliamua Israeli kwa miaka ishirini […]

Waamuzi 11

1 Basi Yefta Mgileadi alikuwa mtu shujaa. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba. 2 Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamaa yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.” 3 Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika […]

Waamuzi 12

Yefta Na Efraimu 1 Watu wa Efraimu wakaita majeshi yao, wakavuka kwenda Zafoni, wakamwambia Yefta, “Kwa nini mmekwenda kupigana na Waamoni bila kutuita ili tuende pamoja nawe? Basi tutaichoma moto nyumba yako, pamoja nawe ukiwa ndani yake.” 2 Yefta akajibu, “Mimi na watu wangu tulikuwa na ugomvi mkubwa na Waamoni, hata ingawa niliwaita hamkuniokoa katika […]

Waamuzi 13

Kuzaliwa Kwa Samsoni 1 Waisraeli wakafanya maovu tena mbele zaBwana. HivyoBwanaakawatia mikononi mwa Wafilisti kwa muda wa miaka arobaini. 2 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Sora, aliyeitwa Manoa, wa kabila la Wadani, naye alikuwa na mke ambaye alikuwa tasa na hakuwa na mtoto. 3 Malaika waBwanaakamtokea huyo mwanamke na kumwambia, “Wewe ni tasa na […]