Waamuzi 14

Ndoa Ya Samsoni 1 Samsoni akatelemkia Timna, akamwona mwanamke wa Kifilisti. 2 Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke wa Kifilisti huko Timna; basi mnipatie ili awe mke wangu.” 3 Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa ndugu zako, hata ulazimike kwenda […]

Waamuzi 15

Kisasi Cha Samsoni Kwa Wafilisti 1 Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia. 2 Huyo baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimkataa, hivyo mimi nikampa rafiki yako. Je, mdogo wake wa […]

Waamuzi 16

Samsoni Na Delila 1 Siku moja Samsoni akaenda Gaza, akamwona huko mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja huku!” Hivyo wakapazingira pale mahali nao wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji. Wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, “Tumvizie hadi mapambazuko, ndipo tutamwua.” 3 Samsoni akalala mpaka usiku wa manane. Akaondoka katikati […]

Waamuzi 17

Sanamu Za Mika 1 Palikuwa na mtu aliyeitwa Mika ambaye aliishi katika vilima vya Efraimu. 2 Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,100za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.” Ndipo mama yake akamwambia, “Bwanana akubariki, mwanangu.” 3 Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama […]

Waamuzi 18

Wadani Wahamia Laishi 1 Katika siku hizo Israeli walikuwa hawana mfalme. Katika siku hizo kabila la Wadani walikuwa wanatafuta mahali pao wenyewe pa kuishi, kwa sababu walikuwa hawajafika kwenye urithi wao miongoni mwa makabila ya Israeli. 2 Hivyo Wadani wakatuma mashujaa watano kutoka Sora na Eshtaoli ili kupeleleza nchi na kuichunguza. Hawa watu waliwakilisha koo […]

Waamuzi 19

Mlawi Na Suria Wake 1 Katika siku hizo Israeli hawakuwa na mfalme. Basi Mlawi mmoja aliyeishi sehemu za mbali katika nchi ya vilima ya Efraimu, akamchukua suria mmoja kutoka Bethlehemu ya Yuda. 2 Lakini suria wake akafanya ukahaba dhidi yake, naye akamwacha akarudi nyumbani kwa baba yake huko Bethlehemu ya Yuda. Baada ya kukaa huko […]

Waamuzi 20

Waisraeli Wapigana Na Wabenyamini 1 Ndipo Waisraeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na wa kutoka nchi ya Gileadi wakatoka kama mtu mmoja wakakusanyika mbele zaBwanahuko Mizpa. 2 Viongozi wote wa kabila za Israeli wakakaa kwenye nafasi zao katika kusanyiko la watu wa Mungu, askari 400,000 waendao kwa miguu wenye panga. 3 (Wabenyamini wakasikia kuwa Waisraeli […]

Waamuzi 21

Wabenyamini Watafutiwa Wake 1 Wana wa Israeli walikuwa wameapa kwa kiapo kule Mispa: “Hapana mtu awaye yote atakayemwoza binti yake kwa Wabenyamini.” 2 Watu wakaenda Betheli, wakaketi mbele za Mungu mpaka jioni, wakapaza sauti zao, wakalia sana. 3 Wakasema, “EeBwana, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limewapata Waisraeli? Kwa nini kabila moja la Israeli […]

Yoshua 1

Bwana Anamwagiza Yoshua 1 Baada ya kifo cha Mose mtumishi waBwana,Bwanaakamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Mose: 2 “Mtumishi wangu Mose amekufa. Sasa basi, wewe pamoja na watu wote hawa, jiandaeni kuvuka huu Mto Yordani kuingia nchi ambayo karibu nitawapa wana wa Israeli. 3 Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile […]

Yoshua 2

Rahabu Na Wapelelezi 1 Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba jina lake Rahabu na kukaa humo. 2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, “Tazama! Baadhi ya Waisraeli wamekuja huku usiku huu kuipeleleza nchi.” 3 Hivyo […]